kuna tofauti kubwa sana kati ya hawa watu wawili, mmoja dikteta mwingine mwana demokrasia, watu hawa hawalinganishwi kwa mambo mengi, na mwafaa alilijua hili mapema akazuia uhuru wa habari, akavibana vyombo vya habari, mihimiri ya bunge, mahakama na vyombo vya haki vikabinywa, akazuia uhuru wa kujieleza, akazuia kukosolewa na akataka asifiwe tu(udikteta). Jk alikua mvumilivu sana aliruhusu watu kujieleza, vyombo vya habari vilikuawa huru, haki za binadamu walikuwa huru, kwa upande mwingine tuliona mkwere kaharibu sana kwakua aliruhusu uhuru huu, hatukuwahi kuona akifunga watu kwa kumkosoa,aliitwa mpaka dhaifu ila kwa ukomavu wa kisiasa alikaa kimya, nakumbuka kauli yake siku moja alisema"jamani unajua raisi ana mamlaka makubwa sana, nikiamua nimwambie mwema kamata hao kina lissu atawakamata" ukimlinganisha na mwafaa...hana uvumilivu kabisa angeruhusu uhuru huo mpaka leo angekua kwenye hari ngumu sana, upepo wa Lowassa asingeuweza kabisa, ... sasa hivi ukiangalia nchi inavyoendeshwa ni one man show...vyombo vya habari haviko huru tena vimebaki kusifia tu...habari ni magufuli atumbua, mkuu wa wilaya aweka mtu rumande..hata ikitokea upinzani wakaitisha press conference tv na magazeti hawatairusha kama ilivo, watakata kata habari wanayodhani itamuudhi mwafaa haitarushwa,mifano tumeiona maiti za watu saba,kupotea Ben,maafa kagera, vyobo vya habari havikutoa uzito kabisa na vilivyoandika ni jujuu tu ili wasimuudhi mwafaa, juzi nilimusikia mama wa haki za binadamu akilalamika wakiomba tv kufanya vipindi vya kuikosoa serikali tv zinakataa... watu wakikosoa wanafungwa na mbaya zaidi hakuna utawala wa sheria tena dhamana mpaka mwafaa atoe ruhusa, tumeona mifano mbunge anakamatwa na katikati ya kesi alipotaka kupewa dhamana hakimu akapigiwa simu na baada ya simu ile maamuzi ya hakimu yalibadilika...baada ya hapo tunayaona yanayoendelea...sehemu pekee iliyokuwa imebaki kuikosoa serikali ni mitandao ya kijamii ..na yenyewe tunaona kina Melo wanayofanyiwa, kwa ufupi tumegeuka taifa la watu waoga, mawaziri waoga, wabunge waoga, wakurugenzi waoga, wanachi waoga, anaogopwa mwafaa, wataalam wetu wamekua waoga hawatumii tena taaluma zao, mtu mmoja ndo mtafiti,Dr,mchumi,hakimu,etc... mwafaa akasema jk we mvumilivu mimi siwezi kuvumilia...raisi hana uvumilivu wa kukosolewa mmmh.. Mungu apishe mbali tusizinguane na nchi yoyote atatupeleka vitani huyu