Tofauti kati ya dalili za mwanamke mwenye kukupenda kama rafiki na mwenye hisia na wewe za kimapenzi

Cheef Baroka

JF-Expert Member
Apr 28, 2019
491
1,002
Wadau miongoni mwa vitu sipendi ni kumtafsiri /kumuelewa mtu tofauti.

Kuna mdada (workmate) ambae ni katika wenyeji walonipokea na kunifundisha pamoja nakunionyesha mazingira ya kazi kazini kwetu.

So kadri siku zinavyoenda ndio tulivyozidi kuzoeana na kuwa karibu zaidi . Nowadays kuna dalili anazionyesha nashindwa kum judge moja kwa moja kuwa anahisia namimi au aninikubari kiushikaji tu.

1: kujichekelesha kila anaponiona.
2: anapenda kunipigapiga tumakofi kila tunapotania au kufurahi.
3: anaweza akaniita afu nikimsogelea hana anachoniambia cha maana.
4: anapenda kujiimbisha nyimbo zakimapenzi anapikuwa karibu na mm.
5: anatamani sana kujua sababu za moods zangu .

Yanayonifanya nisithibitishe kama ana hisia na mimi za kimapenzi au ni ushikaji tu

1: mazoea hayo na ukaribu huo ni tukiwa pamoja2 tukiwa mbali hata sms hanitumii labda awe na shida zake. Na hata niki ntext huchelewa kujibu au hujibu kwa mikato.
2: Nikizungumza neno lolote linaloashalia nina hisia nae huwa ana badilisha mada au analegeuza lionekane lina maana nyingine.
3: Hapendi me nimguseguse au kumshika mwili wake .
4: Ananiita kaka .
5: ananitumia sana kwenye mambo yake kama kumsaidia vikazi vinavyohitaji Nguvu au kunkopesha japo namimi pia huwa ananisaidia napo hitaji msaada wake.

Wakuu naombeni mnieleze nisikurupuke kuhisi ananipenda kimapenzi kumbe ananipenda kama rafiki au mtu wake wakaribu nikajikuta naharibu kila kitu.

Lakini pia naweza hisi ni urafiki kumbe ashakolea afu ananiona nyoka wakibisa.

Je, nini tofauti kati ya dalili za mwanamke anaekupenda kimapenzi na anaekupenda kama rafiki au mtu wake wakaribu.
 
Wabongo tunafeli sana you are friends afu unataka umtongoze pia ofisini yeye ni mwenyeji wako...kuna wengine hizo ni tabia zao,maofisini people hawako serious maana wanaitana baby na utani mwingi ila jichanganye utongoze utatamani uache kazi.

Fanya kazi achana na mapenzi ya ofisini,utakuja ujute maisha yako yote.
 
Back
Top Bottom