Toa maoni yako kuhusu hili ila usivuke mipaka

Karot

JF-Expert Member
Mar 6, 2017
1,159
1,312
Kwa wale tunaohitaji mabadiliko ndani ya chombo hiki, haya ndio aliyoyasema cdf leo!!

1. Kuajiriwa ndani ya chombo hiki kwa darasa la sabana , kidato cha nne mwisho awe na miaka 18. Kwani tunaamini darasa la saba tayari atakua amemaliza akiwa na umri wa miaka 14, ila atakuwa anasubiri muda wa kuwa enroll ambao ni 18. Ambao ni sawa na aliyemaliza kidato cha nne, kama umerudia rudia na akawa na miaka zaidi ya hiyo hataipata hiyo nafasi.

2. Kidato cha sita ataandikishwa akiwa na umri wa miaka 19 hadi 20
Hapa amezingatia kuwa wanafunzi tunaowapeleka nje ya ya nchi kufanya kozi ya o/cadet huwa wanatakiwa wasizidi miaka 19, hivyo TPDF tumekuwa tukipeleka wazee ambao hawafikii kiwango cha kimataifa!

3. Kwa degeree/Advance diploma, watakaoandikishwa umri wao hautazidi miaka 22.

4. Madaktari na wale wenye phd umri hautazidi miaka 27.

Afande mkuu wa majeshi ya ulinzi, ameyasema hayo alipokuwa akiongea na maafisa na askari wa 21 KJ , leo trh 03 Mar 17. Aidha amewakumbusha maafisa na Askari kutunza kiapo chao cha utii, uadilifu na tabia njema, na kwamba hatamvumilia askari au Afisa atakayetenda kosa na kupelekea yeye ndio kuwa kwenye headline ya vyombo vya habari.

Pia alisema ipo haja ya ku restructure mpangilio wa Ikama, na uajiri pamoja na kurejesha misingi iliyokuwa imewekwa imara kuimarisha nidhamu na utii kwa maafisa na Askari. Katika kuelezea hoja hizo, Afande mkuu wa Majeshi alisema kuwa, ipo haja ya kusitisha Vibali vinavyotolewa kwa maafisa na Askari wanapofikisha miaka 25 baada ya kumaliza mafunzo ya recruit au O/Cadet kuruhusiwa kuoa na kuishi nje ya kambi kwani kwa kufanya hivyo maafisa wadogo na Askari wamekuwa hawajui mila na taratibu za mess/Jeshi, ambapo ndipo wanapokutana na wakongwe na kuelimishwa..
Suala la Askari kupandishwa cheo bila kufanya kozi anazostahili za cheo hicho kwa sababu tuu ya degree yake au masters za kozi za uraiani, haitakubalika!! Akitolea mfano wa maafisa waliopelekwa exposure dets mbalimbali , maafisa hao wanakuwa hawana viongozi wa kuwaongoza, kwa kuwa tayari wao wameteuliwa kuwa makamanda wa hizo detachments, na badalaka yake wanaowaelekeza ni nco's ambao nao wamepata madaraka hayo kwa degree zao, ambapo elimu ya kijeshi wanakuwa hawana ya kutosha.... . Hivyo matokeo yake, tutakuwa na jeshi lisilokuwa na weledi wa kutosha.

Muda wa kazi kwa Jeshi zima kuanzia sasa utakuwa ni saa 12 jiobi na itwekwa kwenye FRO, Muda wa kazi utaishia saa kumi jioni na masaa 2 yatakywa ni ya vipindi vya michezo kuanzia jtatu hadi Alhamisi, Ijumaa itabaki kuwa nusu siku. Afande A/LFC Brig SS Othman , Alimshukuru Afande CDF kwa kuliweka wazi, kwani LFC ambao tayari walikwishaanza kutekeleza maagizo hayo walionekana kama wanaonewa na hivyo ku create double standard! Aidha mkuu wa majeshi alitaka muda wa kazi huo urekebishwe kwenye FRO mara moja.

Aidha mkuu CDF alisema upo mpango wa wabajeshi wote kuishi kambini, kwani vitendo vya kuvamiwa na kujeruhiwa maafisa na askari vimezidi kuwa vingi.. Mpango utakaowekwa ni kwamba wale watakaoishi kambini watalipwa maintenance Allowance, na watakaoishi kwebye nyumba zao hawataweza kulipwa chochote, hivyo ni kuwataka wote waishi kambini pale nyumba zitakapopatikana za kutosha.....

Nimechoka kuandika, kama una swali uliza..
Nimesahau.. Na RA fedha zitakuwa chini ya QM, kila utakapokula atakutiki, hutalipwa mkononi..
 
Kudadeki mwafwaa
Yaani ela ya ration iwe kwa kwata master

Ushauri: umeandika vifupi vingi sana wengine hawataelewa, jitahidi kuandika maana zake au usiweke vifupi kabisa ili kumfanya kila msomaji aelewe, namaanisha andika Uzi kwa kutumia
non-technical language
 
Mmmmmhhhhhhh...hilo la Rashidi Abdallah kuwa chini ya QM gumu kumesaaaaaa...!!






Tafakari...!!
 
Back
Top Bottom