Amina Thomas
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 272
- 130
Niko hapa tmj toka saa tatu asubuhi(muda ambao nilipangiwa kufika) dokta ameingia saa tano na robo.! Yaani tumekaa mpaka tunasinzia. Hivi kwa nini umpangie mgonjwa kuja mapema wakati muda wa kuja dokta unajulikana. Maana tukiulizwa tunaambiwa zaa hizi dokta anakuaga hajafika. Yani inakera maana wengine wako hoi, Njaa zinawauma na ukijumlisha na maumivu ndio usiseme. Acheni hizo. Kuweni na mpangilio mzuri.
sasa haya uliyoandika umewambia wao, naona kama unatuambia sisi vile
pole sana mkuu
Kuna Box la maoni hapo kati wanapo pima joto,uzito
tumeshawaambia lakini hawa manesi wanaona ni kawaida. mpaka saa hizi hatujamuona daktari. nikitoka hapa lazima niwatafute wahusika maana nina hasira. mgonjwa wangu anateseka
masanduku ya maoni yako sehemu nyingi sana,ila maoni yanayotolewa yanafanyiwa kazi?sitaki kuamini kuwa uongozi wa hospitali hawajui tatizo.sasa kama wanajua tatizo na hawatatui,unadhani ukiwaandikia watatatua?asante mkuu nimeliona