TLP yataka SMZ imtenge Maalim Seif

TLP yataka SMZ imtenge Maalim Seif

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
1,056
Reaction score
1,086
CHAMA cha Tanzania Labour(TLP) kimemuandikia barua Rais wa Mapinduzi wa Zanzibar, Dk Mohamed Ali Shein na kumtaka kuanzia sasa wamtenge Katibu Mkuu wa CUF , Maalim Seif Sharif Hamad (pichani), kwa kutomualika kwenye shughuli zozote za kitaifa mpaka atakapojirekebisha na kuitambua rasmi serikali iliyopo madarakani.

Aidha, kwa kuwa CUF inadai kwamba haiitambui serikali hiyo basi ruzuku kwa chama hicho isitishwe kuanzia sasa hadi hapo chama hicho kitakapoitambua rasmi serikali hiyo na kuacha kuhamasisha wananchi wasilipe kodi.

Katika barua ya chama hicho iliyosainiwa na Mwenyekiti wake, Augustine Mrema ilisema chama hicho kimesikitishwa na wanalaani kitendo kilichofanywa Hamad ambaye pia alikuwa Makamu wa kwanza wa Rais kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa wa Zanzibar (SUK) wakati wa maziko ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar, marehemu Mzee Aboud Jumbe cha kukataa kumpa Rais Shein mkono wa kusalimiana.

Alisema kuleta tofauti za kisiasa msibani kwa makusudi, Maalim Seif ameendelea kuwagawa Wazanzibari kisiasa na kushindwa kumuenzi marehemu Aboud Jumbe, ambaye pamoja na kuiongoza Zanzibar kwa amani na utulivu pia ndiye aliyemlea Maalim Seif kisiasa.

Alisema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa marudio uliosusiwa na CUF, Maalim Seif amekuwa akileta chokochoko na uchochezi dhidi ya serikali ya Zanzibar akidai kwamba haitambui na kuwataka wananchi wa Zanzibar kugoma na kuwataka wasilipe kodi kwa serikali.
 
Nilitegemea TLP waandike barua ya kumshutumu Jecha, hakika wonders will never end...
 
Kina wabunge wangapi hako ka TLP? Si bora ajiunge tu na ccm.. Sasa maana ya chama cha upinzani ni nini kama kila serikali inachofanya wewe unakikubali..?
 
Dr. Augustine Mrema ni kichwa sana ndio Waziri bora wa Mambo ya ndani na Naibu waziri Mkuu bora wa zama zote.

Ndio Mtanzania Pekee aliewahi kuwa Mbunge katika majimbo tofauti matatu ya Temeke, moshi vijijini na Vunjo.

Ndio Mtanzania pekee aliekuwa Mbunge kupitia vyama tofauti vitatu vya Siasa vya CCM, NCCR Mageuzi na baadae TLP.

Ndio Mtanzania pekee aliekuwa Mwenykt wa vyama tofauti viwili vya Siasa.
Ndio Mtanzania wa kwanza kufukuzwa kutoka uwaziri kwa kuwatetea Watanzania dhidi ya Mafisadi ( kashfa ya Chavda).

Ndio Mtanzania wa Kwanza kupata ujasiri wa kuiambia SMZ kumtenga Mchochezi wa visiwa vya Zanzibar.

Mwnykt bora wa PAROLE wa zama zote kwa kuamua kupunguza msongamano wa wafungwa kwa kushawishi watu wajiepusha na vitendo vya kuwapeleka gerezani badala ya kusubiri wafungwe ndio awasamehe!

Longlife Lyatonga!
 
TLP imekuwa kama genge la wahuni siyo chama cha siasa.
 
Hahahahaha kwi kwi kwi kwi teh teh teh teh siasa za Tanzania ukiwa siriazi sana utakufa kabla ya wakati wako ha ha ha ha hahahahaha
 
Chama chenyewe ni bora ya Viccoba hata faida vinatoa ila si hicho mana wanachama wake hata kujitambulisha ni aibu kwa watanzania wanaweza hisi Umewahi patwa na degedege ukakosa tiba
 
Mrema kila Leo anakuja na mpya na hoja zake zisizokuwa na mashiko yeye vita yake kuu ni upinzani wenzake.
 
Dr. Augustine Mrema ni kichwa sana ndio Waziri bora wa Mambo ya ndani na Naibu waziri Mkuu bora wa zama zote.
Ndio Mtanzania Pekee aliewahi kuwa Mbunge katika majimbo tofauti matatu ya Temeke, moshi vijijini na Vunjo
Ndio Mtanzania pekee aliekuwa Mbunge kupitia vyama tofauti vitatu vya Siasa vya CCM, NCCR Mageuzi na baadae TLP
Ndio Mtanzania pekee aliekuwa Mwenykt wa vyama tofauti viwili vya Siasa.
Ndio Mtanzania wa kwanza kufukuzwa kutoka uwaziri kwa kuwatetea Watanzania dhidi ya Mafisadi ( kashfa ya Chavda)
Ndio Mtanzania wa Kwanza kupata ujasiri wa kuiambia SMZ kumtenga Mchochezi wa visiwa vya Zanzibar
Mwnykt bora wa PAROLE wa zama zote kwa kuamua kupunguza msongamano wa wafungwa kwa kushawishi watu wajiepusha na vitendo vya kuwapeleka gerezani badala ya kusubiri wafungwe ndio awasamehe!

Longlife Lyatonga!
Asante kwa kutumia lugha ya "alikuwa"
 
Angejua nani katengwa Zenji wala asingejisumbua !
Kuna mtu anaongoza dola na chama huku si wananchi!
 
Atapewa wizara ya mambo ya ndani we subiri
 
Dr. Augustine Mrema ni kichwa sana ndio Waziri bora wa Mambo ya ndani na Naibu waziri Mkuu bora wa zama zote.

Ndio Mtanzania Pekee aliewahi kuwa Mbunge katika majimbo tofauti matatu ya Temeke, moshi vijijini na Vunjo.

Ndio Mtanzania pekee aliekuwa Mbunge kupitia vyama tofauti vitatu vya Siasa vya CCM, NCCR Mageuzi na baadae TLP.

Ndio Mtanzania pekee aliekuwa Mwenykt wa vyama tofauti viwili vya Siasa.
Ndio Mtanzania wa kwanza kufukuzwa kutoka uwaziri kwa kuwatetea Watanzania dhidi ya Mafisadi ( kashfa ya Chavda).

Ndio Mtanzania wa Kwanza kupata ujasiri wa kuiambia SMZ kumtenga Mchochezi wa visiwa vya Zanzibar.

Mwnykt bora wa PAROLE wa zama zote kwa kuamua kupunguza msongamano wa wafungwa kwa kushawishi watu wajiepusha na vitendo vya kuwapeleka gerezani badala ya kusubiri wafungwe ndio awasamehe!

Longlife Lyatonga!
Si bure kwa sifa hizi mrema atakuwa babako au mjomba wako.
 
Back
Top Bottom