TISS iongezewe nguvu ilinde maslahi ya nchi/taifa

DOMBWELA

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
757
843
Ijapokuwa sina uhakika sana na majukumu yote ya Taasisi yetu hiyo, zaidi ya kukusanya taarifa za kijasusi na kuishauri Serikali. Sheria au Katiba ikiwezeshe kulinda maslahi pia ya Nchi /Taifa, bila kuangalia ni chama gani, kiongozi gani, kikundi gani, mtu gani anayevunja maslahi ya Nchi/Taifa n.k.

Nasema hivyo kwa sababu nahisi kuwa tumekosa chombo chenye kutimiza jukumu hilo. Inaumiza na kushangaza kuona matukio yanayo kiuka maslahi Taifa yanafanyika na yanapotea kimya kimya sina haja ya kutaja matukio hayo maana ni mengi. Matukio hayo yanayo umiza Nchi/Taifa na vizazi vitakavyo kuja baada ya sisi kupita. Yana puuzwa si kwamba hawa TISS hawa kuwa na taarifa bali ni kwa sababu aliyefanya ni mtu mzito serikalini, ni chama fulani cha siasa, ni mtu wetu, ni Mbunge wetu, ni Waziri wetu, ni Rais wetu n.k.

Kama ni kweli yanafanyika na kuachwa katika mazingira hayo kuna haja ya kuhakikisha maslahi ya nchi/Taifa kulindwa na chombo kama hicho ambacho kitakuwa hakifungamani wa kukubali maslahi ya Nchi/Taifa kupotea ilikuondoka hapa tulipo fikia.

Ndivyo nionavyo mimi, ila sijui wewe unalionaje hili.
 
Sasa TISS imekuwa tawi la CCM,kazi yake ni kuua upinzani kwa gharama yoyote.Imekuwa GESTAPO,chini ya Bashite.
 
TISS ifumuliwe yote. Hii siyo ile TISS ya akina Siyovelwa, Kitine, Membe, na Apson. TISS ya akina Bashite kweli italinda maslahi ya Taifa? Huo ni utani kwa kweli.
 
Najiuliza kwanini vijana wengi wa ufipa mnaiponda tiss? Kwani ndio huwa inapiga kura za kuwakataa? Taasisi ambayo tunaihusisha kisiasa na matukio ya ndani ya vyama vyetu then tunaihukumu kwasababu ya migogoro yetu wenyewe ya uchu wa madaraka....

Tufike pahala tuangalie siasa za vyama vyetu zimekaaje. Lipumba toka 1995 yumo tu anagombea, Seif hadi nguvu zimemuishia anaota kuwa Rais wa Zanzibar.....

Mbowe amewatimua watu wengi tu ndani ya chama kisa aendelee 'kutawala'. Vyama ambavyo leo vinawaaminisha watanzania kuwa flani ni fisadi then kesho vinatwambia huyohuyo mtu ni 'msafi kama malaika'. Hivi vyama havifai hata kidogo.

Watanzania hatujaona mbadala wa CCM. Watanzania tunaona matatizo ya vyama vya upinzani ni kung'ang'ania madaraka na sio TISS. Uzoefu unaonesha wapinzani wakizidiwa hutafuta wapi pa kupeleka lawama zao...
 
Ufipa wanajipiga midole wenyewe alafu wanailalamikia hicho chombo kitakatifu kwa ustawi wa Taifa letu..
 
TISS ifumuliwe yote. Hii siyo ile TISS ya akina Siyovelwa, Kitine, Membe, na Apson. TISS ya akina Bashite kweli italinda maslahi ya Taifa? Huo ni utani kwa kweli.
Hivi kumbe bashite naye ni tiss? Kwa hiyo kumbe mkuu wa mkoa anaweza kuwa tiss
 
TISS ifumuliwe yote. Hii siyo ile TISS ya akina Siyovelwa, Kitine, Membe, na Apson. TISS ya akina Bashite kweli italinda maslahi ya Taifa? Huo ni utani kwa kweli.
wewe ni mjinga sana. heri mtu yule atakaye kupuuza. ufumuke wewe kwanza...
 
TISS ndio sehemu ya kuondolea stress kwa mabavicha.kitu kidogo TISS.hawajau majukumu na nia ya kuanzishwa TISS.
Hao TISS wakiamua kukinukisha hapo chadema mtapigana visu wenyewe kwa wenyewe,lakini kwa kuwa hayawahusu wanafanya ya kwao tu
 
Metsada: Mbona unachukia tunaposema TISS ifumuliwe? Mbona kufanya 'reform' ni jambo la kawaida katika mifumo ya serikali? Hata nyumba ikiwa na hitilafu huwa inabomolewa ndugu.
 
Back
Top Bottom