Timu za Brighton na Newcastle zapanda daraja ligi kuu Uingereza

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Mpaka sasa ni timu mbili tayari zina uhakika wa kucheza ligi kuu ya Uingereza(zimepanda Daraja) nazo ni Brighton na Newcastle

Hii Brighton ni Ngeni kidogo manake tangu nimeanza kufuatilia enzi za Nottigham forest,Leeds,ipswich town,portmouth hawa jamaa hapana.

Newcastle hawa wanajulikana vizuri wakiwa chini ya mtaalamu wa kispain mwenye Uzoefu wa soka la Uingereza wamerudi tena baada ya kushuka msimu uliopita.

Je wataleta mapinduzi kama ya Leicester city tusubiri na tuone,hapa sasa imebaki timu moja ili kujiunga na hizi nyingine.
 
Kwa kuongezea kidogo , Newcastle United wamepanda daraja baada ya kufikisha point 88 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote , na hivyo kuungana na Vinara Brighton &Hove Albion waliokwishapanda siku kadhaa zilizopita

Newcastle imepanda kwa kishindo baada ya kuitandika Preston North End 4 - 1 , kwa mabao mawili ya Ayoze Perez , bao tamu la Christian Atsu na lingine la penati ya Matt Richie .

Naipongeza sana Newcastle baada ya kufaninikiwa kuchoropoka kwenye ligi ngumu sana ya Championship na kudumu kwa msimu mmoja tu .
 
Acha uongo.. championship haiwez kuwa league Ngumu... hata siku moja..
 
Newcastle ina mapungufu makubwa matatu , beki wa kati , kiungo mkabaji na mshambuliaji wa ukweli .

Bila kurekebisha haya mtarudi mlipotoka .
Mtaalam benitez yupo atarekebisha.tukirudi championship naendelea na Chelsea yangu.
 
Back
Top Bottom