Timu nne kupanda daraja VPL

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257

​

Timu nne zinatarajiwa kupanda Ligi Kuu Tanzani Bara msimu ujao huku timu mbili pekee msimu huu zikishuka daraja ili kuweza kuandaa mpango mpya wa msimu wa mwaka 2015/2016, ambapo timu 16 ndizo zitakazoshiriki ligi hiyo.

Kwa sasa ligi kuu ina timu 14 pekee, ambazo zinashiriki na kila msimu zilikuwa zikishuka timu tatu pekee na kupanda tatu kutoka daraja la kwanza.

Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Silas Mwakibinga, amesema kuwa msimu ujao ni timu nne kutoka daraja la kwanza ndizo zitakazopanda na msimu huu mbili zitashuka.

Mwakibinga alisema mpango huo utaanza msimu ujao na kwa sasa waliopo daraja la kwanza wanatakiwa kuonyesha bidii kwa kiasi kikubwa kuhakikisha wanafanikiwa kupanda.

"Timu nne msimu ujao ndizo zitakazopanda ligi kuu na mbili msimu huu ndizo zitakazoshuka, bidii na uwezo wako wa kupata pointi kihalali ndiyo vitakufanya kutoka chini kuja juu na wengi itawabidi warudi huku chini na kujipanga upya," alisema Mwakibinga.

Kabumbu
 
Sio mbaya tusubir tuone Ashanti united, Mwadui fc, Kanembo jkt na jkt orijolo wakirudi tena ligi kuu...
 
Sio mbaya tusubir tuone Ashanti united, Mwadui fc, Kanembo jkt na jkt orijolo wakirudi tena ligi kuu...
Vipi kuhusu Tessema, African Lyon, Pannone, Kurugenzi, MAjimaji n.k.?

Yote tisa, mimi sizipendi hizi timu za majeshi kwani ni vigumu kuwa na mipango endelevu kwa kuwa kila kambi inaweza kuwa na timu yake. NApenda timu za raia zaidi....
 
Vipi kuhusu Tessema, African Lyon, Pannone, Kurugenzi, MAjimaji n.k.?

Yote tisa, mimi sizipendi hizi timu za majeshi kwani ni vigumu kuwa na mipango endelevu kwa kuwa kila kambi inaweza kuwa na timu yake. NApenda timu za raia zaidi....
Upo sahihi kabisa mkuu, hizi timu za jeshi ni mizinguo tu!! kwann hizi timu za majeshi zisiunganishwe zikatengeneza timu moja imara!!!
 
Upo sahihi kabisa mkuu, hizi timu za jeshi ni mizinguo tu!! kwann hizi timu za majeshi zisiunganishwe zikatengeneza timu moja imara!!!
Wenzao Kenya wana timu moja ya Jeshi la Ulinzi, inaitwa Ulinzi Starz...
 
toto africa,and african sports com up to join stand united against mbumbumbu fc
 
Nilichogundua kuna timu zina majina madogo na yasiyojulikana mnazisahau kujadili, Timu ya Kimondo ssc Ina kiwango kizuri na uwezo wa kuingia ligi kuu!
Ndiyo timu iliyomudu mfumo wa usajiri mpya uliotolewa na FIFA katika muda uliotolewa na Tff hapa si timu za ligi kuu ama za daraja la kwanza.
-Ina wachezaji wana uwezo na umri mdogo na uwezo kwenye mikakati yake kufikia malengo yake!! Ni timu ambayo kwenye msimu uliopita ilifanya vizuri kwenye michezo ya ugenini zaidi kuliko ya nyumbani( kutokana na hii ilitokana na uwanja wa nyumbani kuingiliana na politic na tofauti zilizosahihishwa na sasa imekuwa moja ya timu zinazokuja kwa staili ya Mbeya City)
Ni timu ya wananchi, ambapo wilaya za Momba na Mbozi wamekubali kuijenga ili wanapopata mkoa wa Songwe rasmi wawe na timu ya ligi kuu. Jambo hili limefanikiwa kutokana na wafanyabiashara wengi Tinduma kujitokeza kuimwagia mamilioni kwenye safari yake
Kissc is comming!
 

Tunazisahau kuzijadili kutokana na media zetu uchwara, watu hawawezi kujadili ambacho kwenye vyombo vya habari havipo. Kila mshabiki anajadili upuuzi ule ule wa akina Jaja na Okwi na sio vitu vya maana kwa kuwa vyombo vyetu vya habari ndio vimeamua hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…