Timu hazifungwi kwa bahati mbaya kwa Mkapa.

Vhagar

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
20,064
38,946
Natumai mmeamka salama,


Hizi fikra zilianza kujengeka tangu mechi za mnyama hasa kuanzia mechi na js saoura.
Ikafika mbali mpaka kuonekana kuwa eti tunapulizia timu pinzani sumu ya kulegeza misuli. Sasa imefikia mpaka mechi ya jana wengine eti wanasema kuwa Uganda wametuachia, wanashindwa hata kuangalia mpira tuliocheza na mashabiki walivojitokeza hadi kuvunja geti.

Hivi walioweka sheria pia ya faida ya goli la ugenini walikuwa wapuuzi? Wao wenyewe wanajua jinsi gani ilivyo ngumu kupata matokeo away.
Now tukubali wote kuwa kwa kiasi fulani mpira wetu unakuwa na timu zetu zinajua jinsi gani ya kutumia faida ya uwanja wa nyumbani ambao zimeuzoea.
Mpira wetu wa Afrika ndivyo ulivyo timu zote zinapigana kufa na kupona kushinda kwake na si kingine. Tuache wachache wanaobaki na ujinga vichwani wakidhani mpira wa Tanzania haubadiliki, mimi nathubutu kusema kuwa sasa unabadilika na tunaona, Simba imesonga mbele, na Tanzania imesonga mbele kwa faida kubwa ya kutumia uwanja wa nyumbani kama timu zingine.

troublemaker 2019. all right received.
 
Back
Top Bottom