Wamarekani wana ubabe wa kipumbavu sana. Hawataki maendeleo ya wengine
Kutukana hovyo ni dalili ya kukosa akili. Ukiona unapenda kutukana sana, ujue kichwani hakupo sawa.
Ungesoma vizuri, uelewe kabla ya kuanza kutoa maneno ya kashfa. Hao Wamarekani, kama Serikali yao itachukua hiyo hatua, ni dhahiri serikali yao itakuwa inaongozwa na watu wenye akili sana, watu wanaowajali watu wao.
Marekani haijaizuia Tiktok kufanya biashara Marekani, lakini wanataka wananchi wao, ambao ndio wateja wa hiyo Tiktok, ambao ndio watakaoitengenezea faida Tiktok, nao washiriki kwenye sehemu ya faida wanayoitengeneza. Yaani Tiktok ijiandikishe kwenye soko la hisa la USA, ili nao waweze kununua hisa.
Kama hujui, Wachina wanawazuia watu wao kutumia Whatsapp. Ukipatikana unatumia, ni kosa, unaadhibiwa!! Hilo hulishangai?
Saudi Arabia, ukiwekeza mradi wako wowote, ni lazima ushirikiane na wasaudia, hilo hulishangai?
Nchi zinazjitambua, zilizobahatika kuwapata watawala wenye akili, wanaotaka wananchi wao wafaidike na chochote wanachochangia kukinawirisha, ndivyo wanavyofanya.
Nchi zinazoongozwa na viongozi waliokosa uelewa na wasiojali wananchi wao, kama wa hapa kwetu, mgeni anaweza kuja, anaanzisha kampuni ya kuvuna rasilimali, na wala hauzi hisa hapa kwetu, lakini anauza hisa Toronto Stock Exchange, Sydney Stock Exchange, London Stock Exchange; huku watanzania wakiwa hawana habari, wanashindana namna ya kumsifia mama!!!