Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,802
- 34,193
Singida: Jeshi la Polisi mkoani Singida limemtia mbaroni Monica Munishi (22), mkazi wa Sabasaba, Singida ambaye ni mwalimu ‘ticha’ wa Kanisa la Anglikana kwa kosa la kutupa kichanga chooni kwa mchungaji aitwaye Kanon Mpilimbi.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo lililojiri hivi karibuni, maeneo ya kanisa hilo lililopo Kata ya Mghanga, Mchungaji Mpilimbi (62) alikuwa akielekea maliwatoni na ghafla akashtushwa na sauti ya kichanga akilia.
“Mchungaji alikuwa anaingia maliwatoni, alipoingia ndani ndipo akasikia sauti ya kichanga huyo ikitokea katika shimo la choo.
“Baada ya hapo alifuata tochi kwa kuwa kulikuwa na giza ndani ya kile choo ndipo tukabaini kuwa ni kweli kichanga alikuwa ametupwa,” kilisema chanzo.
Iliendelea kuelezwa kwamba, kabla hawajachukua hatua yoyote ya kumtoa, walitoa taarifa polisi ambapo walirudi na kumtoa kichanga huyo na kubainisha kuwa ni wa kiume huku sehemu kubwa ya mwili wake ikiwa imechafuka kwa kinyesi.
“Baada ya hapo tulimpeleka katika hospitali ya mkoa ambako anaendelea na matibabu hadi sasa,” kilisema chanzo chetu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kuendelea na mahojiano juu ya mtu huyo wanayemshikilia.
chanzo.Ticha mbaroni kwa kutupa mtoto chooni kwa Mchungaji