Tiba ya chronic nematodes

LUOLE

Member
Oct 17, 2012
8
1
nimekuwa nikisumbuliwa na aina mbalimbali za nematodes tangu mwaka 2005.Nimetumia dawa mbalimbali lakini bado tatizo lipo na huwa naambiwa hao nematodes wamekuwa sugu mpaka wanatengeneza cyst , naombeni ushauri
 
Mkuu, Pole...lakini Nematodes ni group kubwa ya viumbe(kibaiolojia huitwa Phylum
ingekuwa rahisi kama uki-specify Nematodes wa aina gani ulioamviwa guko hospitali)...

Ila tatizo hasa ni minyoo(nematodes) kwa ujumla kwa kutumia dawa za minyoo huweza kutibu tatizo, Ushauri wa daktari pia ni muhimu kwani minyoo hao huweza kuishi umbali hata wa mita 30 kutoka usawa wa ardhi na umbali wa mita 50(urefu) kutoka mazalia yao, hivyo uvaaji wa viatu, usafi wa maji na vyakula na matunda, usafi binafsi(kabla na bada ya kula, kutoka uani.n.k).
 
Nashukuru mkuu,kila mara madaktari wanasema nina trichuris na giardia worms .Nimetumia dawa mbalimbali hata za kuharibu cyst lakini bado tatizo lipo.
 
Nashukuru mkuu,kila mara madaktari wanasema nina trichuris na giardia worms .Nimetumia dawa mbalimbali hata za kuharibu cyst lakini bado tatizo lipo.

Pole mkuu, lakini ELIMU kuhusu ugonjwa huu unapatikanaje ni muhimu, ukiwa kwa daktari wako muulize hasa shida ni nini...kwani mtu hupata minyoo hiyo, ikizaliana, kumbuka ugonjwa huu hupatikana kwa njia ya chakula (Feacal -Oral transmission), yaani kwa kiwango kidogo kilicho katika uchafu kama nilivyokuwa nimeeleza awali, hujirudia.Hivyo unaweza kutibiwa na ikaonekana kama tatizo linawezekana likaisha...lakini ukarudi katika mazingira au mazoea YALE YALE na hivyo kufanya tatizo lionekane sugu.

Kwa kutumia dawa za minyoo na antibiotics huondoa tatizo.
 
Back
Top Bottom