DAWA ASILIA YA MALARIA SUGU
[TABLE="width: 702, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Majani Ya Aloe Vera
Kama unasumbuliwa na Malaria Sugu fuata maelekezo yafuatayo kutayarisha dawa ya asili.
MAHITAJI :
i. Majani ya mwarobaini kiasi cha viganja viwili vya mtu mzima.
ii. Majani ya Aloevela kiasi cha viganja viwili vya mtu mzima..
iii. Maji safi na salama lita tatu.
Hatua Za Kufuata
Changanya majani ya mwarobaini na alovela kwenye sufuria, kisha ongeza lita tatu za maji safi na salama halafu chemsha pamoja mpaka utakapo ona mchanganyiko wako unatoa mchuzi ama soup. Ipua , chuja, kasha ihifadhi dawa yako kwenye chupa ya chai.
:
Kunywa kikombe kimoja cha dawa yako mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu mfululizo na malaria itapona.
ALTERNATIVELY :
Vile vile unaweza kutumia ndimu na maji ya madafu kujitibu malaria sugu.
i. Ndimu Saba Zilizo komaa vizuri.
ii. Maji Ya Madafu.
JINSI YA KUFANYA :
Chukua dafu, likate kisha maji yake uyahifadhi kwenye jagi, halafu chukua ndimu saba, zikamulie kwenye maji ya madafu halafu koroga mchanganyiko wako.
MATUMIZI :
Kunywa glasi mbili kwa siku, asubuhi glasi moja na jioni glasi moja. Fanya hivyo mpaka malaria itakapo ondoka.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
UKIWA NA SWALI AU TATIZO LOLOTE UNAWEZA KUNITAFUTA KWA KUBONYEZA HAPA. Mawasiliano
ikisha poa utakunywa...Kunywa kikombe kimoja cha dawa yako mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu mfululizo na malaria itapona.nashukuru sana mkuu,,kwahyo unainywa ikiwa ya moto km chai ama unaeza kuipoza kidogo unywe km maji?
ikisha poa utakunywa...Kunywa kikombe kimoja cha dawa yako mara tatu kwa siku kwa muda wa siku tatu mfululizo na malaria itapona.
Majani ya aloe vera !!!!!!!!!! ufafanuzi MziziMkavu aloe vera inamajani au yale madude yake ndio majani ???????
dah aisee mkuu kumbe ni chungu kupita maelezo,,nimefanikiwa kunywa nusu kikombe tu,,jion ntajaribu kumaliza chote
Hakuna namna yoyote ya kupunguza huu uchungu mkuu?? MziziMkavu
Ndio Majani yenyewe Unatumia njia hii hapa chini angalia picha.yale ndo majani yenyewe mzee
Uchungu ndio Dawa yenyewe inavyofanya kazi tumia nusu kikombe au kipimo cha kikombe cha kahawa inatosha kabisa.dah aisee mkuu kumbe ni chungu kupita maelezo,,nimefanikiwa kunywa nusu kikombe tu,,jion ntajaribu kumaliza chote
Hakuna namna yoyote ya kupunguza huu uchungu mkuu?? MziziMkavu