SoC02 Tiba halisi ni kubadili mifumo ya maisha

Stories of Change - 2022 Competition

Erny1165

Member
Jul 31, 2022
8
5
Mpaka sasa takwimu zinaonyesha ongezeko la vifo katika umri mdogo na milipuko ya magonjwa hatarishi vimeendelea kuongezeka kwa kasi kubwa sana kote duniani, ila changamoto kubwa zaidi zimekuwa zikiyakuta mataifa ya dunia ya tatu yaani "Third world countries" kwa lugha ya kighaibu ikimaanisha mataifa yanayoendelea, mara zote sababu zimekua zikiripotiwa kuwa ni mabadiliko ya tabia nchi inayochagizwa vikali zaidi na maendeleo ya kiteknolojia.

Yamkini inaweza kuwa kweli lakini tujiulize ni kwanini mataifa yanayoendelea na sio zaidi kwa mataifa yaliyoendelea kama jamhuri ya Uchina, ambayo inaripotiwa kuwa na takwimu ndogo sana ya watu wanaokufa wakiwa na umri mdogo lakini pia milipuko ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ambukiza ni ndogo, je huko hakuna maendeleo ya kiteknolojia? Je hakuna mabadiliko ya tabia nchi? Jibu ni hapana, sasa kwanini kwenye mataifa yetu?

Basi leo kwa pamoja tutizame sababu kubwa knayoendelea kutafuna watu kwenye mataifa haya ya dunia ya tatu.

Sababu yenyewe si nyingine bali ni mifumo ya maisha ambayo tumechagua kuishi.

Awali mababu zetu waliishi katika mifumo mizuri ambayo iliwafanya kuwa imaara na wenye afya hali iliyowafanya waishi kwa muda mrefu tukichukulia mfano wa watu ambao wanajulikana na vijana wengi akiwemo Bibi Kidude (marehemu) lakini pia hata Alli Hassan Mwinyi ambaye bado yuko hai hadi sasa.

Kwa namna moja ama nyingine tunaweza laumu mifumo ya kiteknolojia ambayo imetuletea mabadiliko makubwa ya mifumo yetu ya maisha na matokeo yake yamekuwa ni kutodhoofisha, lakini tujiulize ni nani aliyetulazimisha kufata mifumo hiyo?? Jibu ni hakuna.

Hakika tutakuwa mashahidi watu wengi wanakufa kwa magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kama vile mashinikizo ya damu, kisukari, matatizo ya figo, maini n.k ambayo yote hayo yanasababishwa na mifumo ya maisha ambayo tumeichagua.

Leo hii hakuna Mtanzania aliye tayari kutumia dawa zetu za asili kusuluhisha matatizo ya kiafya aliyonayo ukiuliza atakwambia hizi hazijathibitishwa anataka dawa za mahospitalini kisa zimeandaliwa na mataifa ya ulaya au Marekani bila kujua madhira makubwa yaliyo kwenye madawa yale.

Babu zetu waliumwa na kujitibu kwa dawa hizihizi ambazo leo tunaambiwa hazina uthibitisho kama zinaponya na wakati huohuo ukifatilia mataifa ya India na Jamhuri ya Uchina wanaosifika kwa kuponya magonjwa makubwa yanayosumbua sana wanatumia dawa asilia.

Leo hii vijana wa kiafrika hatuko tayari kula vyakula vya kiasili ambavyo vina virutubisho vyote stahiki kama vile mihogo ya kuchemsha , magimbi, ndizi, mboga zinazoandaliwa bila mafuta mengi badala yake tunakimbilia chipsi ambazo zina rundo la mafuta bila kufikiria athari zake kiafya.

Vijana wa sasa kwenye suala la mazoezi imekuwa ni changamoto kiasi kwamba kijana anashindwa kutembea hata mwendo wa kilomita 5 na wakati babu zetu walitembea mpaka kilomita 40 watu sasa hivi tunakimbilia magari tukisahau kuwa yanatufanya kuwa wazembe na matokeo yake tunaweza ishia kupata maradhi na kudhoofisha miili yetu.

Tafiti zinaonyesha vyakula tunavyokula mara nyingi vina kiwango kikubwa cha wanga na mafuta, tunapokula bila kushughulisha sana miili yetu matokeo yake ule wanga utafanyika kuwa sukari (glucose) na kutunzwa mwilini hatimaye kuugua maradhi kama kisukari na pia yale mafuta yanaweza kupelekea kuwa na maradhi ya shinikizo la damu (presha) magonjwa ambayo yanahusishwa kuua watu wengi kupita maelezo.

Aidha vijana wengi kwa sasa wanaendekeza sana unywaji wa pombe kupita kiasi, matumizi ya sigara, bangi, mirungi na aina nyingine za vilevi wasifikirie wanaweka mazingira mabaya kwa viungo muhimu kama vile maini, mapafu na figo unakuta kijana hata hajafikisha miaka 50 ana matatizo ya maini na figo kutokana na mfumo mbovu wa maisha anayoyaishi.

Mifumo hii hii ya maisha inawapeleka vijana pabaya zaidi kwani wengi sasa hivi wanapenda kuiga unakuta kijana amejichora mwili mzima matatuu hatima yake unakuja kusikia anasumbuliwa na kansa za damu, ngozi nk na mwisho wake mara nyingi ni vifo katika umri mdogo.

Hapo mwanzo nilisema sababu kubwa inayotajwa juu ya vifo katika umri mdogo na ongezeko la magonjwa ni mabadiliko ya tabia nnchi lakini ukiangalia kiundani unakuta hata mabdiliko ya tabia nchi bado ni matokeo ya mifumo ya maisha tunayochagua, kutokana na uzembe na uvivu tulio nao vijana kwa sasa imepelekea vitu vingi sasa vinafanywa kwa kutumia mashine ambazo matokeo yake ni uchafuzi wa mazingira na hewa ambavyo huchochea zaidi mabadiliko ya tabia nchi.

Je, ni nini sasa kifanyike?

Kuna mambo kadha wa kadhia yanayoweza kufanyika ili kurudisha ile hali iliyokuwepo hapo awali kipindi cha babu zetu.

Kwanza mifumo ya vyakula na madawa tunayotumia inabidi ifanane na ile waliyotumia wazee wetu, tuache kuiga mifumo ya waghaibu na badala yake yupende kula vyakula vyetu vya asili vilivyoandaliwa kiasili na turudi kwenye matumizi ya dawa zetu asilia kama vile miarobaini, alovera, vivumbasi, asali, vitunguu saumu n.k kwani hivi maranyingi havina madhara ya kikemikali lakini pia tafiti zinaonyesha dawa hizi zinatatua kuanzia kwenye mzizi wa tatizo tofauti na madawa ya viwandani.

Lakini pia tutizame namna babu zetu walivyoandaa vyakula vyao kiasilia hivyo kufanya chakula kuwa salama zaidi kwa mfano kwa jamii za wahaya chakula kinaandaliwa kwenye jani la mgomba ambalo halina athari kama zilizopo kwenye sahani za plastiki na bati zinazotumika zama hizi, lakini pia vyakula vilipikwa kwa kutumia vyungu ambavyo havina madhara kiafya.

Pia vijana inabidi tupunguze uvivu na uzembe tujitahidi kushughulisha miili yetu ili vyakula tunavyokula vitumike na sio kurundikwa ndani ya miili hatimaye kuzalisha magonjwa hatarishi aidha kushughulisha mwili kunasaidia sana kuziamsha seli hai nyeupe ambazo husaidia kupambana na maradhi lakini pia husaidia kuondoa sumu kwenye miili yetu.

Maendeleo ya kiteknolojia yamefanyika ili kutusaidia lakini tunapoyaendekeza kupita kiasi ndipo yanatuletea madhira hivyo basi vijana ifike hatua tupunguze matumizi ya vitu kama vile simu, kompyuta na televisheni ambavyo hutoa miyonzi mikali inayoweza kupelekea matatizo kama vile kansa, matatizo ya mifumo ya neva na hata matatizo ya kuona na kusikia.

Kwa kuhitimisha nitoe wito kwa serikali kupitia wizara ya afya na asasi zote zinazoshughulika na masuala ya afya waweze kuandaa mafunzo semina na warsha mbalimbali ili kuelimisha jamii za vijana vijanano wa moja kwa moja uliopo baina ya afya zao na mifumo ya maisha hii itasaidia kuwarudisha vijana kwenye mstari bora kwa manufaa ya taifa zima kwani vijana ni nguvu kazi ya jamii.

Kiuhalisia tutazunguka dunia nzima tukitafuta tiba ila tiba halisia tutakuwa tunazunguka nayo ambayo ni mifumo ya maisha tunayoyaishi hii ndiyo chanzo cha tatizo na ndio suluhisho pia.

Kumbuka: Kula vyakula vilivyoandaliwa vizuri, kula matunda na mboga mboga asilia, tumia dawa asili, fanya mazoezi na kuushughulisha mwili, pata maji safi ya kunywa mara kwa mara, punguza matumizi ya vifaa vyenye kutoa miyonzi... Utanishukuru baadae

Ni mimi mtumishi wa wote
ERNEST MODEST MPIRA
 
Naombeni kura zenu hii ni makala inayolenga kuleta mabadiliko chanya kwenye fikra za vijana ili kuweza kubadili mifumo ya kimaisha na kuepuka maradhi yasiyo ya kuambukizwa ambayo yameendelea kumaliza watu wengi sana duniani kama vile shinikizo la damu, kisukari na kansa
 
Naombeni kura zenu hii ni makala inayolenga kuleta mabadiliko chanya kwenye fikra za vijana ili kuweza kubadili mifumo ya kimaisha na kuepuka maradhi yasiyo ya kuambukizwa ambayo yameendelea kumaliza watu wengi sana duniani kama vile shinikizo la damu, kisukari na kansa
Naunga mkono hoja,.lakini kumbuka Hali ya maisha ndiyo inayoamua mfumo wa maisha kiongozi.
 
Naunga mkono hoja,.lakini kumbuka Hali y
Naunga mkono hoja,.lakini kumbuka Hali ya maisha ndiyo inayoamua mfumo wa maisha kiongozi.
Mfumo wa maisha unaamuliwa na wewe mwenyewe kwani leo hii tuna watu wana hali duni za kimaisha lakini kutokana na mfumo walioamua kuishi wana afya nzuri ama kuliko watu wenye maisha ya hali ya juu.
Lakini pia kwenye kundi hilohilo la watu wenye hali duni wapo wenye changamoto za kiafya kutokana na mfumo waliouchagua
Changamoto kwa wengi ni wanaacha kuchagua mfumo ulio bora kwa afya zao badala yake wanachagua mfumo unaoonekana kuwa bora kwa watu
Mtu anaona akiwa na hela ili aoneshe watu basi ale "Junk foods" bila kufikiria madhara yake kwa afya anataka watu wamwone waseme ana maisha bora kumbe anajidanganya.
 
Back
Top Bottom