thread : tushirikishane maandiko ya biblia hapa kila siku

shelumwa

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
516
189
najua watu siku hizi wamekua busy kiasi kwamba hata biblia hatusomi sasa hii thread ni kwa ajili ya mtu yoyote mwenye neno au andiko la kushikiana na watu wengine hasa ya biblia .

mimi naanza kama hivi nawe pia unaruhusiwa kutuma maandiko yako ili kushibisha nafsi na roho zetu kila siku


ufunuo 22:12
tazama naja upesi, na ujira wangu u pamojq nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.

ufunuo 22:20
yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, naam ; naja upesi. amina nq uje bwana YESU.

mathayo 4:4
naye akajibu akasema, imeandikwa, mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha MUNGU.

ufunuo 22:21
neema ya Bwana YESU na iwe pamoja nanyi nyote, Amina.
 
Back
Top Bottom