Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,183
- 7,300
Uzi huu utakuwa uzi maalum wa tetesi zote za usajili katika kulekea msimu mpya wa ligi kuu na michuano ya kimataifa 2026\2027.
Tutakuwa tunapata taarifa timu ipi itamsajili mchezaji gani au kocha kwa sababu zipi kiufundi na matokeo yake yatakuwaje.
Leo tunaanzia hapa
===========
Mabingwa wa kihistoria wa soka nchini Tanzania, Young Africans, wameendelea kuonyesha umwamba wao katika dirisha la usajili baada ya kufikia makubaliano rasmi ya kumsajili winga machachari na mzoefu, Heritier Luvumbu Nzinga, kutoka klabu ya AS Vita ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.
Taarifa zinaeleza kuwa Yanga imekuwa ikimfuatilia kwa karibu nyota huyo wa kimataifa wa DR Congo kutokana na uwezo wake mkubwa wa kucheza pembeni, kasi yake akiwa na mpira, pamoja na uzoefu wake wa kucheza mechi za ushindani wa juu ndani na nje ya Afrika.
===============
KLABU ya Simba imeanza rasmi mazungumzo ya chini kwa chini na Menejimenti ya mshambuliaji wa Azam FC, Abdul Hamisi Suleiman maarufu kama Sopu, kwa lengo la kuinasa saini yake kuelekea msimu wa 2026,27, huku mabosi wa Msimbazi wakitajwa kuvutiwa zaidi na uwezo wake wa kushambulia kutokea pembeni pamoja na kasi yake akiwa kwenye eneo la mwisho la ushambuliaji.