Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
THOMAS Ngawaiya, alikuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kilimanjaro amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa madai ya kufanya shughuli za ujenzi wa ghorofa kinyume cha sheria namba 17 kifungu 22(4) ya ukandarasi ya mwaka 1997.
Akisoma kesi hiyo namba 322, Saddy Kambona, Wakili wa Serikali mbele ya Warialwande Lema, Hakimu Mkazi amesema kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 24 Machi, 2015 katia Mtaa wa Dosi na Wazani, Magomeni Dar es Salaam.
Kambona amesema, Ngawaiya alitumia wajenzi wasio wakandarasi waliosajiliwa na bodi ya wakandarasi nchini kujenga jingo la hoteli lenye thamani ya zaidi ya Sh. 500 milioni. Mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana ambapo kesi hiyo itatajwa tena tarehe 20 Aprili mwaka huu.
Naona wenye viburi wa nchi hii waanza kutiwa jamba jamba.
Source: Mwanahalisi