Hilo ni jambo la kawaida hususani kwenye hizi nchi zetu za kiAfrika.
Kwa nchi zingine za wenzetu kwa kiasi fulani Tawala za huko zimejitahidi kuweka Mazingira fulani wezeshi ya kuweza kuwapunguzia maumivu Watu wasio na kazi au wasio na ajira hususani Vijana.
Ipo mipango na miradi mbalimbali ya kuwawezesha vijana kujikimu kimaisha,
Kwa Afrika hali ipo tofaufi kabisa, janga la Ukosefu wa Ajira linawafanya Waathirika kupata maumivu ya moja kwa moja bila ya msaada kutoka kwa Serikali, rejea kisa Cha Kuibuka kwa Machafuko katika nchi za kiArab (Arab Uprising) yaliyotokea miaka ya 2011-2015 katika nchi za Tunisia, Libya, Misri, n.k. Trigger iliyosababisha janga hili lote ni Ukosefu wa Ajira, Utawala wa Tunisia ndio ulioanza kufungua milango ya vurugu kwa kubomoa banda la biashara la Kijana Mchuuzi wa biashara ndogo ndogo (Machinga)