This is 2020. What went wrong?

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Kila mwaka huanza ukiwa mpya na wenye kuleta furaha na nyuso za tabasamu katika kila mmoja wetu.

Lakini matarajio huwa tofauti pale matatizo yanapoanza kuiziba na kuinyima matumaini furaha iliyokuwepo mwanzo.

Nahisi huu kwetu ni mwaka mrefu zaidi na wenye historia wakati huo itabidi niwasimulie wajukuu ntakao kuwa nao kwa nukta.
Haya ni baadhi ya matukio makubwa ninayoyakumbuka mpaka sasa.

1. Corona: Mnamo miezi mitatu ilipita hivi tangu mwaka kuanza ndipo hapo. Jamii ilipoanza kuufuta katika fikra ule usemi wa "huu ni mwaka wako. Ugonjwa wa homa ya mapafu(COVID-19)ulianza kurindima nchini China. Umbali ukawa kigezo cha watu kupuuzia.Lakini baada ya muda Afrika ikashuhudia kuenea kwa ugonjwa huo ukianzia nchi za Magharibi(West Africa)hatimaye ukaingia Afrika ya Mashariki.

Kufuatia kuenea huko hatua mbalimbali zikaanza kuchukuliwa kulinda maisha ya watu wasio na hatia. Shule za sekondari na msingi hata vyuo vikafungwa kuepusha msongamano lakini pia shughuli zote zinazotegemea mkusanyiko Kama vile michezo na matamasha ya burudani yalizuiliwa kwa kipindi.Barakoa na kunawa mikono haikutosha kuwa tahadhari pekee. Bali hata kujifukiza na kutumia njia ambayo kila mmoja aliamini ingemnusuru zikiwemo za kula Tangawizi,malimao na kujifukiza.

2. Black Lives Matter: Hizi ni harakati za MTU mweusi kudai haki yake zilizopamba moto huko Marekani.

Kufuatia tukio la mauaji ya Mzungu Mweusi George Floyd aliyeuawa na polisi May 25, 2020 huko Minneapolis. Tukio hili liliibua hisia za watu wengi duniani katika kudai haki ya mtu mweusi. Maandamano mfululizo ya watu mbalimbali huko Marekani yaliyotokea yalipelekea kuchafuka kwa mambo huku masanamu ya wakoloni waliokuwa wakifanya biashara ya utumwa yakibomolewa na kutupwa majini.

3. Kifo cha Benjamini Mkapa: Kifo cha Hayati Benjamini Mkapa aliyekuwa raisi wa awamu ya tatu kilichotokea July 24, 2020.
Alifikwa na umauti alipokuwa hospitali akiuguzwa maradhi ya moyo(heart attack) alikuwa kati ya maraisi shujaa barani Afrika walioleta mabadiliko katika uchumi wa nchi na katika mifumo ya kifedha.

Aliboresha miundombinu na kuleta usawa na haki katika demokrasi ya nchi hii. Hakika atakumbukwa na kuenziwa na watanzania daima.

4. Vita dhidi ya Marekani na Iran: kufutia kifo cha Qasem Soleimani aliyekuwa mkuu wa ulinzi wa Iran. Vita dhidi ya Irani na Marekani ilichukua sura mpya na dunia ilipata mashaka wenda ikawa ndio mwanzo wa dalili ya vita ya dunia(World War 3)

Matukio mengine yaliyotikisa dunia kwa mwaka huu ni:
5. Kifo cha Kobe Bryant
6. Shambulio la kigaidi la Beirut

Kwa mashabiki wa soka nao mwaka 2020 haujawaacha nyuma

7. Sakata la Bernard Morrison
8. Yanga kuifunga Simba mbele ya Rais
9. Simba kulipiza kisasi
10. Madrid kuifunga Barcelona El classico

Kwa wadau wa siasa nao mwaka 2020 Umekua gumzo kwao.

11. Joto la uchaguzi Octoba 28
12. Kurejea kwa Lissu Tanzania
13. Fumbo la kufikia Uchumi wa Kati

Lakini pia katika jamii mwaka 2020 haukuwaacha bila neno
14.Laizer kuwa Bilionea Tanzania
 
Mkuu hizo ni changamoto tuu ila huu ni mwaka mzuri sana ,yaani bado kuna mengi mazuri yanakuja.kuwa tayari kuyapokea
 
2020 na majanga yake
Screenshot_20200823-065706.jpg

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Bila kusahau upande wa wasanii
1.Uchebe kutemwa na shishi food

2.Zuchu kulipwa milioni 20 kwa shoo. .

3.Na Babu tale kufiwa na msiba kufanyika kwao kwenye nyumba ambayo hata panzia la 7,000 Ni msiba wa wapili.
 
Back
Top Bottom