Unarejea kuuliza kwa kuwa umekarii jibu la "sijui" lakini Mimi nafahamu kuwa uwezo wote na ujuzi wote unahusisha kuumba ulimwengu wa aina yoyote. Kama uwezo wote kwako ni kuumba ulimwengu wa aina Fulani.Siwezi kuacha kuuliza swali ambalo hujalitatua.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujalitatua hili swali, na siachi kukuuliza mpaka ulitatue au kukubali kwamba hujui utatuzi wake.
Sijakataa kwamba uwezo wote unajumuisha kuumba ulimwengu wowote.Unarejea kuuliza kwa kuwa umekarii jibu la "sijui" lakini Mimi nafahamu kuwa uwezo wote na ujuzi wote unahusisha kuumba ulimwengu wa aina yoyote. Kama uwezo wote kwako ni kuumba ulimwengu wa aina Fulani
Huo ni uwezo wote kwa "time and space " na sio kwa Moral God.
Waona aibu kwa kuwa udhaifu wa swali lako umewekwa peupe wenye fikra wote wanauona hivyo ili kulinda udhaifu wako umekomaa ati huoni majibu kwenye majibu unayopewa.
Ulidhani kuamini Mungu hayupo ni kwa wenye akili kumbe ni kwa wenye uwezo mkubwa wa kukariri huku hekima ikitumika kiduchu.
Swali lako la kwanini kaumba ulimwengu wa aina hii linatokana na wewe kuhoji juu ya uwezo wake, kwa akili yako pungufu unafikiri uwezo wote ungeonekana angeumba ulimwengu unaoupenda wewe. Mimi sina tatizo na ulimwengu huh ambao wewe unakutatiza kwa kuwa hutaki kutumia hekima aliyokupa.Sijauliza mipaka ya uwezo wake ni ipi.
Nimeuliza kwa nini kaamua kuumba ulimwengu aliouumba.
Hujajibu swali ambalo umeulizwa.
Swali ambalo umelijibu hujaulizwa.
Kwa nini unaongelea uwezo wakati mimi swali langu si la uwezo, ni la sababu?Swali lako la kwanini kaumba ulimwengu wa aina hii linatokana na wewe kuhoji juu ya uwezo wake, kwa akili yako pungufu unafikiri uwezo wote ungeonekana angeumba ulimwengu unaoupenda wewe. Mimi sina tatizo na ulimwengu huh ambao wewe unakutatiza kwa kuwa hutaki kutumia hekima aliyokupa.
MTU mwenye tafakari ya kweli hawezi kuuliza swali la kwanini kaumba ulimwengu aina hii huku akikataa majibu ya wanaofahamu kuhusu uumbaji na sababu zake na anaendelea bila aibu kukomaa na swali ambalo amepewa majibu japo hayapendi kwa kuwa yanamwonyesha alivyo mtupu kichwani.
Kwanini kaamua kuumba ukimwengu wa aina hii.
Jibu: Kwa sababu iko ndani ya uwezo wake kuumba ulimwengu wa aina hii na kuwapa binadam hekima ya kuutumia kwa manufaa yao.
Wewe ndiwe huelewi, kwa mfano wako huo wa tajiri ni sawa na kuhoji kwamba tajiri kwa nini kanunua nyumba iliyojengwa kwa miti badala ya kununua nyumba ya matofali ya saruji ?Kwa nini unaongelea uwezo wakati mimi swali language si la uwezo, ni la sababu?
Unaelewa tofauti?
Mtu akiwa milionea, Ana uwezo wa kuumba nyumba yoyote, lakini akanunua nyumba Coco beach, mimi nikaja kuuliza, high mtu Ana uwezo wa kununua nyumba yoyote, kwa nini akanunua nyumba Coco beach? Hapo nitakuwa nimehoji uwezo wake wa kununua nyumba au sababu zilizomfanya anunue nyumba Coco beach?
Nikianza kwa kusema kuna tajiri ana uwezo wa kununua nyumba yoyote, siwezi kukuuliza swali la uwezo wa Huyo tajiri kununua nyumba, kwa sababu hilo nimeanza kwa kulikubali as a setup to my question.Wewe ndiwe huelewi, kwa mfano wako huo wa tajiri ni sawa na kuhoji kwamba tajiri kwa nini kanunua nyumba iliyojengwa kwa miti badala ya kununua nyumba ya matofali ya saruji ?
Sasa kwa akili yako pungufu unasema nisizungumzie uwezo wake wa kununua nyumba yoyote atakayo popote bali nizungumzie sababu za uamuzi wake !
Nawe wajiona mzima kichwani kwa viroja hivyo ?
Sababu umewekewa isipokuwa uwezo wa kuelewa hunaSijakataa kwamba uwezo wote unajumuisha kuumba ulimwengu wowote.
Swali langu halihoji uwezo wa mungu wako.
Ukiongelea uwezo, unaniambia kwamba uwezo wako wa kuelewa ni mdogo sana, ndiyo maana huwezi kunijibu.
Swali langu linasema, huyo mungu wako mwenye uwezo wote, alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.
Hakuumba ulimwengu huo.
Kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.
Swali langu ni, kwa nini kaumba ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana na hajaumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Ukinijibu kwamba mungu ana uwezo wote kwa hiyo hilo linajumuisha hata ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, unaonekana hujaelewa swali langu.
Swali langu haliulizi uwezo wa mungu huyo.
Linauliza sababu zake za kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana.
Unazijua? Unaweza kuzitaja?
Swali nililouliza mimi si la uwezo, ni la sababu.Kwa akili yako pungufu uamuzi wa kufanya au kutofanya jambo hauwezi sababishwa na uwezo ?
Kwa hiyo alishindwa kuumba ulimwengu ambao binadamu atautawala bila ya ulimwengu huo kuruhusu mabaya?Sababu umewekewa isipokuwa uwezo wa kuelewa huna
Narejea. Aliumba ulimwengu wa a in a hii ili binadam autawale hivyo aliumba wa aina hii kwa ajili ya wanadam wapate nafasi ya kutumia hekima aliyotupa juu ya namna ya kuutumia ulimwengu na vitu vyote vilivyomo...
Swali nililouliza mimi si la uwezo, ni la sababu.
Jibu lake hujanipa.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujajibu swali hili.
"Kukubaliana kutokukubaliana" is an oxymoron and a waste of space.
Nimekuuliza, mungu alishindwa kuumba ulimwengu ambao watu watautawala bila ya ulimwengu huo kuwa na mabaya?Sababu umewekewa isipokuwa uwezo wa kuelewa huna
Narejea. Aliumba ulimwengu wa aina hii ili kwakuwa pamoja na kuumba ulimwengu alimuumba binadam ambaye alimpa ujuzi au hekima ya namna ya kuutawala na kuutumia ulimwengu huu kwa faida yake.
Hivyo aina hii ya ulimwengu ndiyo inatimiza kusudi la Mungu kumuumba mwanadamu ili kupitia fahari za ulimwengu na hekima aliyompa apate utukufu.
Utarudi kwenye default position yako kutaka sababu za kuumba ulimwengu wa aina hii ?
Anataka apewe sababu ya kwa nini Mungu alitumia uwezo wake kuumba ulimwengu ambao yeye haupendi. Haoni tatizo kwenye hoja yake
Hapana.Anataka apewe sababu ya kwa nini Mungu alitumia uwezo wake kuumba ulimwengu ambao yeye haupendi. Haoni tatizo kwenye hoja yake
Kakomaa anataka sababu...
Teh jamani,hilo swali jepesi?"Kukubaliana kutokukubaliana" is an oxymoron and a waste of space.
Huyu anazunguka, swali jepesi tu linamshinda kujibu.
Jepesi as in straightforward in its logic. Not in being easily soluble.Teh jamani,hilo swali jepesi?
Swali ni gumu,na ni gumu zaidi pindi unapomuuliza average theist!