The shameless tribe that foisted the killing of babies a.k.a. abortion on humanity exposes itself

Sikumbuki kusikia watu wa Mungu wakitumwa eti 'Katangazeni habari mbovu, sijawahi kuona'....

Labda nijuze kimstari kinachoashiria hivyo nisaidie miwili mitatu. Enlighten me
Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza; kwa kuwa hukumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote; kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza. Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa BWANA, Mungu wako; katika mazingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako.
Kum 28:45‭, ‬47‭-‬48‭, ‬53 SUV


NENO LA MUNGU HILO
 
NENO LA MUNGU HILO
Mh, basi kila mtu na vile anavyoiona na kuichukulia dunia. Basi siwakatazi kushadadia hizo habari lakini mtambue tu 'atupaye tope humrukia' [Daah! ni miaka sasa sijaandika methali ya kiswahili asee!!]. Endeleeni na misheni yenu after all kila mmoja afanye kazi yake, tunajenga nyumba moja. Basi ndugu wewe mwenyewe kaipitie tena hiyo WAEFESO sura ya tano ukitilia mkazo aya ya 3, 4, 10, 12 tuone yepi tunayopaswa kutilia mkazo kama wakristu.

Nimeona hata signature yako inasema 'An honest politician is as rare as an empathetic burglar'

Hayo ni matokeo ya habari zoote ulizowahi kuzisikia kuhusu wanasiasa na wezi hadi hivi sasa. Fikiria kama habari za wanasiasa wazuri zingekuwa nyingi mtaani. Unadhani ungetolea wapi hilo wazo la kujumuisha hivyo? Na hizo habari njema zipo ukizitafuta utaziona.

Sasa habari nzuri za wanasiasa tutazipatia wapi kama kila mmoja atakuwa bize kusambaza tu habari mbovu za wanasiasa? Na habari njema za hao wanawake tutazipata wapi kama kila mmoja atakuwa bize kusambaza habari zao mbovu tu?

Je kazi ya waamini Mungu, ni kuifanya dunia iwe mahali salama? au ni kuifanya iwe uwanja wa fujo? Je tukio hilo unalolifanya linaongeza amani na upendo duniani? au linasambaza chuki na kushukiana duniani? Je linaleta afya au linaongeza magonjwa na presha kwa watu? Mwisho mwishoni inabakia kwenye maamuzi binafsi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom