Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,018
- 20,489
Yote haya yalikuwa yamefanywa wakati wa kipindi cha Cliton, “kitu gani
kinakusumbua sana siku hizi? Boren alimwuliza Tenet asubuhi hiyo. “Bin laden,”
Tenet alijibu akimanisha kiongozi wa ugaidi Osama Bin laden raia wa Saudi
Arabian aliyekuwa akiishi ukimbizini Afghanistan ambaye alikuwa ameanzisha
mtandao wa Al Qaeda dunia nzima neno ambalo kwa kiarabu linamaanisha “
Kituo kikuu”.
“Oh, Tenet!” Boren alisema kwa muda wa miaka miwili iliyopita alikuwa
akisikiliza wasiwasi wa rafiki yake kuhusiana na Bin laden,je, mtu mmoja
binafsi angewezaje bila ya kutumia utajiri wa serikali ya kigeni akawa tishio
kubwa kama hili? aliuliza, “huwezi kufahamu uwezo na kiwango cha yale
wanayoyapanga”, Tenet alisema.
Boren alikuwa na wasiwasi kwamba rafiki yake alikuwa ameamua kuwa na chuki
za ajabu dhidi ya Bin laden. Karibu miaka miwili hapo nyuma muda mfupi tu
kabla ya sherehe za kutimia kwa mwaka 2000 Tenet alikuwa amechukua hatua
ambayo haikuwa ya kawaida kwa kumwonya binafsi Boren asisafiri au kutokea
kwenye matukio makubwa ya wazi katika mkesha wa mwaka mpya kwa sababu
alitegemea kungekuwa na mashambulizi makubwa.
Na siku za karibuni zaidi, Tenet alikuwa na wasi wasi kwamba kungekuwa na
mashambulizi wakati wa sherehe za tarehe 4 Julai 2001. japokuwa hakuyafichua
hayo kwa Boren, kulikuwa na matukio 34 ya habari zilizonaswa miongoni mwa
washirika wa Bin laden zikielezea matamshi kama vile “siku ya kiama ni kesho”
au “ “tukio la ajabu ni kesho”
Kulikuwepo na unaswaji mkubwa wa habari kama hizi katika mitandao ya
ujasusi na ripoti nyingi zilisema kulikuwa na shambulio kubwa dhidi ya balozi za
marekani au dhidi ya makundi ya watalii wa marekani nchi za nje, lakini habari
za kijasusi hazikuweza kufahamu ni lini wapi na kwa njia gani. Hapakutokea
chochote, lakini Tenet alisema kwamba suala hilo lilikuwa linamfanya akose usingizi.
Ghafla mara walinzi wa Tenet walikuja mbio kuelekea mezani alikokuwa.Uh-oh,
Boren aliguna moyoni “Bwana Mkurugenzi”, mmoja wao alisema “kuna tatizo
kubwa”. “Ni nini”” Tenet aliuliza akionyesha kwamba kwake ilikuwa ni vyema
kumpa mtu uhuru wa kuzungumza bila woga . “mnara wa kituo cha Biashara
umeshambuliwa.” Mmoja wao alimpa Tenet simu ya mkono na akapiga simu
makao makuu.
“Kumbe wameigongesha ndege kwenye jengo lenyewe?” Tenet aliuliza akiwa
haamini. Aliamuru watu wake muhimu kukutana katika chumba cha mkutano
kwenye makao makuu ya CIA, Akaagiza kuwa angekuwa amefika huko katika
kipindi cha dakika 15 hadi 20. “Yote haya siku zote yamekuwa ni Bin Laden,”
Tenet alimwambia Boren. “Lazima niondoke” pia alifahamu kwamba uwezekano
halisi ni kwamba CIA na shirika la upelelezi la Marekani (FBI) havikufanya yote
yanayotakiwa ili kuzuia shambulio hilo la kigaidi.”
24
“Nashangaa,” Tenet alisema, “iwapo hii inahusiana na jamaa huyu ambaye
anachukua mafunzo ya kurusha ndege.” Alikuwa akizungumza kuhusu Zacarias
Moussaoui raia wa Ufaransa mwenye asili ya Morocco ambaye FBI ilikuwa
imemtia kizuizini huko Minnesota mwezi uliopita baada yakuonyesha tabia za
ajabu wakati akiwa katika shule ya mafunzo ya kurusha ndege.
Tukio hilo la Moussaoui likiwa bado liko katika mawazo yake. Mnamo Agosti, FBI
ilikuwa imeomba CIA na wakala wa Usalama wa Taifa kufuatia simu zote
ambazo Moussaoui alikuwa amezipata nchi za nje. Mtu huyo alikuwa tayari faili
lake limetuna makaratasi ya unene wa inchi tano katika ofisi hiyo ya ujasusi
wakati Tenet anaingia katika gari lake kwenda kwenye makao makuu ya CIA
ambayo yana eneo la hekta 258 huko Langley Virginia, juhudi zake za kupigana
dhidi ya ugaidi wa siku za nyuma zilikuwa zikipishana kichwani mwake.
CIA ilikuwa inamwinda Bin laden kwa zaidi ya miaka mitano na juhudi hizo
zikazidi baada ya ulipuaji mabomu wa mwaka 1998 wa balozi wa Marekani
nchini Kenya na Tanzania ambao ulisimamiwa na Bin laden na kuacha watu
zaidi ya 200 wakiwa wamekufa. Wakati huo, Rais Clinton alielekeza jeshi la
Marekani kufyatua makombora 66 katika kambi za magaidi ambako Bin laden
anasadikiwa kuwa alikuawa akifanya mkutano muhimu . Lakini ni wazi alikuwa
ameondoka masaa machache kabla ya makombora hayo kufika sehemu hiyo.
Mwaka 1999, CIA ilianzisha harakati za siri za kutoa mafunzo kwa makomandoo 60
kutoka katika shirika la ujasusi la Pakistan ili kuingia Afghanistan kumteka Bin
laden. Lakini harakati hizo zilikwama kutokana na mapinduzi ya kijeshi
yaliyotokea nchini Pakistan. Njia nyingi zaidi na za hatari zilikuwa zimepangwa
katika mfululizo wa mikutano na maofisa wa ngazi za juu wa usalama wa taifa
katika utawala wa Clinton.
Moja ya chaguo ambalo lilikuwa limefikiriwa lilikuwa ni shambulio la usiku
kutoka kwenye helikopta dhidi ya Bin laden kwa kutumia kikosi kidogo maalum
cha Marekani chenye watu wapatao 40, shambulio hilo lingehitaji ndege
kupatiwa mafuta zikiwa angani kwani helkopta hizo zingelazimika kusafiri kiasi
cha maili 900.
Lakini mpango huo ulivurugika kutokanaka na oparesheni “Desert One” ya
mwaka 1980 ambayo Rais Carter aliamuru ifanywe ili kuwaokoa mateka wa
Marekani waliokuwa wanashikiliwa nchini Iraq ambapo ndege kadhaa zilianguka
jangwani na kuangushwa, kama helikopta mbili aina ya “Black hawk” nchini
Somalia mwaka 1993 na kusababisha vifo vya Wamarekani 18.
Jeshi lilisema kwamba shambulio dhidi ya Bin Laden lingeweza kushindwa na
kusababisha hasara kubwa kwa askari wa Marekani, Habari za kijasusi pia
zilionyesha kwamba Bin Laden alikuwa akifuatana na familia yake, na Clinton
alikuwa anapinga oparesheni yoyote ambayo ingeweza kuua wanawake na
watoto.
25
Kikosi maalum cha Marekani na askari wa jeshi la maji wenye uwezo wa
kurusha makombora aina ya ‘cruise’ waliwekwa katika tahadhari lakini walihitaji
masaa sita hadi kumi kuweza kupata tahadhari ya mahali alipokuwa Bin Laden.
Moja ya siri zenye kulindwa zaidi katika CIA ilikuwa ni ile ya mawakala 30 wa
kijasusi wa Afghanistan waliokuwa wakiendesha shughuli zao chini ya maneno
ya siri GE/SENIORS, ambao walikuwa wamepewa fedha kwaajili ya kufuata
nyendo za Bin laden nchini Afghanistan. Katika miaka mitatu iliyopita kundi
hilo ambalo lililipwa dola 10,000 kila mwezi liliweza kusafiri pamoja au
kugawanyika katika vikundi vidogo vya watu watano. CIA kila siku ilikuwa na
vyombo salama vya mawasiliano “the Seniors” kama walivyokuwa wakiitwa, na
walikuwa wamenunuliwa magari na pikipiki lakini kuzifuatia nyendo za Bin laden
likawa jambo gumu zaidi kwani aliweza kusafiri bila mpangilio na kila mara
akiondoka nyakati za usiku au kuwalamba chenga za visigino akipita milimani.
Kitu cha ajabu ni kwamba seniors hao waliweza kujua wakati wote mahali
alipokuwa lakini kamwe hawakuweza kutoa habari thabiti za vitendo yaani
kusema kithibiti kwamba angeendelea kukaa mahali hapo kwa muda unaotakiwa
ili kuweza kulenga makombora ya ‘cruise’ mahali hapo. Na CIA ilishindwa kupata
mtu wa kuaminika ili kufanya ujasusi miongomi mwa watu wa Bin laden ambaye
angeweza kuwadokeza kuhusu mipango yake.
Kulikuwa na watu katika utawala wa Clintoni na vyombo vya usalama wa taifa
walikuwa hawana imani na seniors kwa vile kuna wakati kulikuwa na habari za
kupingana kuhusiana na mahali alipokuwa Bin laden. Na nchini Afghanistan watu
hususani wenye kuleta habari za kijasusi walikuwa wananunuliwa na kutoa
habari kwa watu wengine .Hadi sasa, si Clinton au Bush waliokuwa wametoa
madaraka kwa CIA kutuma seniors au mawakala wengine wenye kulipwa
kwenda kumuua Bin laden. Amri ya kirais kupiga marufuku mauaji ambayo
ilisainiwa kwanza na Rais Gerald Ford , ilikuwa na nguvu ya kisheria.
Katika kipindi kimoja kiongozi wa Seniors wa Afghanistan alikuwa amekutana
mara kadhaa na mkuu wa kituo cha CIA kutoka Islamabad, Pakistan, ambaye
alikuwa anawapa maelekezo na kuwalipa. Kiongozi huyo wa seniors alidai
kwamba walikuwa wameurushia risasi msafara wa Bin laden katika matukio
mawili katika kujihami, jambo ambalo lilikuwa linaruhusiwa lakini alitaka
kuufuatilia msafara huo kwa njia nyingine akiwa anapendekeza kuvamia kwa
kushitukiza ambapo kitu chochote kilicho karibu kitapigwa risasi, kuua kila mtu
na kisha kukimbia.Mkuu wa kituo cha CIA alisema, Hapana hamuwezi kufanya
hivyo jambo hilo litavunja sheria za Marekani.
Kwa kutilia maanani fedha iliyokuwepo, vitengo mbali mbali vya siri na
mazingira yaliyokuwepo, Tenet aliona kwamba CIA ilikuwa imefanya kila kitu
kilichotakiwa kufahamika. Lakini kamwe hakuomba kubadilishwa kwa sheria
alikuwa hajamwambia Clinton kuwepo kwa mfumo wa kijasusi ambao
ungewaruhusu Seniors kumvamia kwa kumshambulia Bin laden.
Mwanasheria kwenye Wizara ya sheria Ikulu aliamini wangekataa na kusema
kwamba hali hiyo ingekuwa imevunja sheria ya kupiga marufuku mauaji ya
26
watu. Tenet aliona amefungamanishwa na msimamo wa Clinton na washauri wake.
Kila kitu kimefungiwa “sheria ya kufa”, alikuwa akisema lakini na yeye pia
alikuwa amechangia katika hali hiyo katika kipindi chake cha miaka mitano na
nusu akiwa kama mkuu wa habari za Ujasusi wa Clinton na Naibu wa idara hiyo.
Sheria ilikuwa inasema kwamba CIA ingeweza kumkamata Bin laden na kumfikisha
katika vyombo vya sheria. Operesheni kubwa ya kufanya kazi hiyo iliwekwa katika
ratiba za njama siri za idara hiyo. Tenet alikuwa ana amini kwamba Bin laden
asingekubali kuchukuliwa akiwa hai, hivyo operesheni kama hii, iwapo
ingefanikiwa, ingepelekea katika mauti yake.
Lakini wataalam wote wa CIA katika kurugenzi ya Uendeshaji walifikiri
isingefanya kazi na kwamba ingesababisha watu wengi kuuawa na si lazima
awemo Bin laden.
Na Tenet alikubali Mpango huo kamwe haukuendelea zaidi ya hapo.
Pendekezo la Saudi Arabia kwamba CIA iweke silaha maalum katika mizigo ya
mama wa Bin laden ambaye alikuwa anasafiri kutoka Saudi Arabia kwenda
kumwona mwanaye nchini Afghanistan, pia lilikataliwa kwa vile lingekuwa la
hatari na kwamba lisingefanikiwa.
27
CRAIG KELLY AMPA UJUMBE POWELL.
Huko mjini Lima, Peru, asubuhi hiyo, waziri wa mambo ya Nje Colin L. Powell
alikuwa ndiyo kwanza ameanza kupata kifungua kinywa na rais mpya Alejandro
Toledo. Powell alikuwa anahudhuria mkutano wa nchi za umoja wa Nchi za
Amerika. .Alikuwa na mategemeo ya mawasiliano mema na mawaziri wa nchi za
nje au viongozi 34 wa nchi 35 za eneo hilo.Cuba ilikuwa haikukaribishwa,
Toledo alikuwa anasisitiza kuhusu mgao wa soko wa nguo kutoka Marekani .
Alitaka kuondolewa kwa kodi katika pamba ya hadhi ya juu ambayo alidai
isingeweza kushindanishwa na pamba ya hadhi ya chini iliyokuwa inazalishwa
katika mataifa ya kusini ya Marekani ambayo ilikuwa inataka pawepo mgao huo
katika soko.
Ghafla mlango ukafunguliwa na Craig Kelly, msaidizi mtendaji wa Powell,
aliingia haraka akiwa na ujumbe uliokuwa umeandikwa katika kipande cha
karatasi kilichokuwa kimechanwa kutoka katika kitabu cha kumbukumbu .Ndege
mbili zimejibamiza katika kituo cha Biashara cha kimataifa .
Ndege mbili, si tukio la ajali, Powell alitambua .ujumbe wa pili ulisema kwamba
ndege hizo zilikuwa ni za injini ya “jet” .Powell akafikiri, nilazima niende nyumbani.
Hata kama kimetokea nini, hali ilikuwa ni mbaya mno kwake kuendelea kukaa katika
mkutano wa mawaziri wa mamboya nje mjini Peru. “Hebu tayarisha ndege,
alimwambia Kelly, Nenda kawaambie tunasubiri”.
Ingechukua kiasi cha saa moja kuitayarisha ndege, hivyo Powell aliueleza mkutano
huo. Mawaziri wengine walitoa hotuba za kumpa pole.Powell alizungumza kwa
ufupi, akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwa pole zao na kuahidi kwamba
Marekani inachukua hatua mara moja “Mkasa mkubwa sana umeikumba nchi
yangu,” alisema “Lakini….lazima mfahamu kwamba Amerika itapambana na
wakosaji watafikishwa mbele ya haki. Mfahamu kwamba pamoja na siku hii kuwa
mbaya kwetu, nilazima tutashinda kwani sisi ni taifa lenye nguvu na linalo jiamini
duniani’ Wajumbe wengine walisimama nakupiga makofi.
Mara tu baada ya ndege kuondoka Powell alifahamu kwamba asingezungumza na
mtu yeyote kwavile vyombo vyake vya mawasiliano vilikuwa vimeunganishwa na
mfumo wa mawasiliano nchini Marekani ambao ulikuwa umejaa habari mbalimbali
za ma wasiliano. Bila yasimu au barua pepe, alikuwa ni sawa na mtu ambaye hakuwa
na nchi. Baada ya dakika kadhaa alikwenda mbele ya ndege kupiga mawasiliano ya
radio. Hiyo ilimaanisha mawasiliano hayo hayakuwa na usalama. Alimpata Richard
L Armitage, naibu waziri wa mambo ya nje na rafiki yake mkubwa, walizungumza
mara kadha, lakini mazungumzo ya maana hayakuwezekana.
Armitage ambaye alihitimu chuo cha jeshi la maji mwaka 1967 alikuwa
ametumikia jeshi mara nne nchini Vietnam na baadaye akawa Naibu waziri wa
ulinzi katika utawala wa Reagan. Alikuwa ni mtu mwenye kupenda kusema
ukweli mwenye tambo kubwa na kifua kipana ambaye hakupenda kuzungumzia
diplomasia yenye kujificha.
28
Hata kabla hawajawa wakuu wa wizara ya mambo ya nje Powell na Armitage
walikuwa wakizungumza mara kadhaa kila siku. “Mtu huyu ninamwamini kuhusu
uhai wangu, watoto wangu, hadhi yangu, kila kitu ambacho ninacho,” alikuwa
akisema Powell kuhusiana na Armitage. Katika mambo yote ambayo Powell
alikuwa anayachukia, ni kushindwa kuchukua hatua yoyote wakati wa tatizo
ndilo jambo lililokuwa linashika nafasi ya kwanza.
Jambo kuu katika upangaji wa sera za usalama wa taifa, na timu ya Ikulu au ya
usalama wa taifa ingetaka kuweka msimamo gani katika upangaji wa sera
kulikuwa kuna utaratibu wa kipekee katika nyakati za matukio makubwa. Hali ya
migogoro ndiyo ilitoa fursa ya kuwepo hatari kubwa zaidi na fursa kubwa zaidi
za utendaji wa kazi. Ni mmarekani wa kwanza mweusi kuweka historia ya
kuhudumu katika ngazi za juu za utawala wa Marekani
Akiwa na umri wa miaka 64 katika kipindi cha mgogoro Powell alikuwa tayari
amekaa katika viti vitatu vya chumba cha dharura vya Ikulu ambavyo ni
mshauri wa kitaifa kwa Rais Regan kwa muda wa mwaka mmoja, kisha akawa
mwenyekiti wa Muungano wa Wanadhimu kwa Rais Bush wa kwanza wakati wa
vita vya Ghuba, na wakati mgogoro alikuwa ni Waziri wa mambo ya nje kwa rais
George W. Bush.
Ripoti nyingine ilifuata ikisema kwamba makao makuu ya jeshi yalikuwa
yameshambuliwa, na kulikuwa na ripoti na uvumi usioaminika kwamba kulikuwa
na ndege nyingine zikiruka kila mahali. Powell alianza kuandika notisi kwa ajili
ya matumizi yake, aliandika hivi, “Watu wangu watakuwa na majukumu gani”?
Je, ulimwengu na Marekani zitajibu vipi tukio hili? Je, hali itakuwa vipi kwa Umoja
wa Mataifa? Je, Umoja wa kujihami wa NATO? Je, nitaanzaje kuwaita watu mbali
mbali wakusanyike? Masaa saba kutowasiliana na mtu yeyote yalionekana kama
miaka isiyohesabika kwa mtu huyo ambaye angekuwa mkuu wa majeshi.
Mnamo 1995, miaka miwili Powell akiwa amestaafu kutoka jeshini, alikuwa
amefikiria kugombea urais. Aliandika kitabu cha simulizi ya maisha yake
kiitwacho My America Journey (Safari yangu ya Amerika) ambacho kilishika
nafasi ya kwanza kitaifa katika idara ya mauzo. Alikuwa amejichimbia katika
siasa za Marekani akiwa katika kiwango cha makadirio ya juu kiumaarufu
ambacho uteuzi wa chama cha Repblican ulikuwa ni wa kutaka aseme tu, na urais
alikuwa karibu sana kuufikia.
Armitage alikuwa amekipinga kitu hicho kwa nguvu “hapana haja. “Achana nacho”
alimshauri rafiki yake huyo, “sidhani kama uko tayari kwa kitu kama hicho”.
Shughuli ya kuendesha kampeni ni jambo ambalo Powell alikuwa halipendi,
“inajumuisha kila kitu kibaya unachoweza kukifikiria.” Powell alikuwa anapenda
mipango iliyotayarishwa vyema utaratibu mwema wenye kuweza kutabirika, na
kiwango cha uhakika jambo ambalo halikuwa ni sehemu ya siasa za haraka haraka
za Marekani.
29
Ilikuwa inafahamika wazi kwamba mkewe, Alma, alikuwa hapendi jaribio hilo
kugombea nafasi hizo. Kilichokuwa siri ni kwamba Alma alikuwa amemwambia
wazi kwamba iwapo angegombea urais angemwacha. “Ukigombea tu naondoka”,
alisema. Alma alikuwa anaogopa kwamba (mumewe) angeshambuliwa au
kupingwa risasi. Mumewe kugombea urais, “akishinda” na yeye kuwa mke wa rais
ni mambo ambayo mwanamke huyo alikuwa hayataki maishani mwake .
“Itabidi uyafanye mambo hayo peke yako,” alisema.
Baada ya Bush kushinda uteuzi wa kugombea urais wa chama cha Repblican
mwaka 2000, Powell alisaini makubaliano ya kutoa msaada, lakini Karl Rove
aligundua kwamba kampeni hiyo ilikuwa ifanye juu chini kumwezesha aonekane
katika tukio lolote sambamba na Bush. Karibu wafuasi wote muhimu wa
Repblican walikubaliana kwamba chaguo la kugombea urais siyo Powell. Watu
wake walitaka kufahamu ni nani mwingine ambaye angekuwepo kwenye tukio
muhimu la chama hicho, kitu gani kingesemwa, nani wangehudhuria, na lengo la
kisiasa lilikuwa nini. Yote haya yalikuwa yamepangwa kuelekeza mgawanyiko
dhidi ya Powell na si Bush.
Isitoshe ni nyenzo za kumweka Bush katika siasa za mlengo wa kati na baadaye
akawa ndiye chaguo kuu la kuwa waziri wa mambo ya nje iwapo Bush
angechaguliwa kuwa rais. Katika sura ya nchi zaidi kulikuwa na hisia kubwa kuwa
walifahamu kuwa walikuwa wanachagua timu si Bush na makamu mgombea
mwenza wake, Waziri wa ulinzi wa zamani Dick Cheney, pia Powell. Wakati
mahakama kuu ilipomtangaza Bush kuwa mshindi kwa kura 537 katika
mkanganyiko wa uchaguzi huko Florida washauri wa Powell walikuwa na imani
kwamba bosi wao alikuwa amesaidia kwa kiwango kikubwa sana katika ushindi
huo.
Katika miezi yake ya kwanza akiwa waziri wa mambo ya nje Powell alikuwa
hajaliziba pengo la uhusiano wake na Bush ambalo halikuwafanya wawe karibu
zaidi kama alivyokuwa na uhusiano wa karibu na watu wengine. Kulikuwa na
pengo kati ya watu hao wenye kuunganishwa na maelewano ya kirafiki. Bush na
Powell walikuwa wanataniana wakiwa na watu wengine lakini walifanya hivyo
mara chache sana wakiwa wawili. Rove alihisi kwamba Powell alikuwa anajidukiza
mno kisiasa na kuendesha shughuli zake nje ya cheo chake. “Lazima ufahamu siku
zote kwamba vyote hivi ni siasa na mimi ndiye nitaushinda mchezo huu wa
kisiasa,” Rove alimwambia kwa faragha Powell.
Kila mara Powell alipokuwa katika mandhari ya mbele kuhusiana na suala fulani
na kuonekana kuwa ndiyo sura ya utawala,shughuli za kisiasa na mawasiliano
huko Ikulu zilihakikisha zina mweka pembeni mwa mandhari na mwanga wa
kisiasa. Rove na Karen P. Hughes mkurugenzi wa muda mrefu wa mawasiliano
wa Bush ambaye wakati huo alikuwa ni mshauri Ikulu waliamua nani miongoni
mwa viongozi angetokea katika kipindi cha mazungumzo cha jumapili kipindi
maarufu cha televisheni kuhusu habari za jioni na asubuhi. Iwapo Ikulu
isingetoa taarifa kupendekeza kwamba akubali mwaliko wa kutokea kwenye
kipindi hicho Powell alikuwa anafahamu utaratibu mzima. Aliwaambia
watayarishaji wa kipindi hicho.
30
Mnamo Aprili 2001 wakati ndege moja ya ujasusi wa kijeshi ya Marekani aina ya
EP-3E ilipokingamwa na ndege za kivita katika pwani ya China, ikalazimishwa
na serikali ya China kutua na kukamatwa mateka wote 24 waliokuwa katika
ndege hiyo. Ikulu ilikuwa imedhamiria kuona kwamba Bush hajihusishi na suala
hilo ili rais huyo asionekane kuwa mzungumzaji katika mgogoro huo. Ilikuwa ni
kama vile hapakuwepo na mgogoro wa mateka, hii ilikuwa ni kwa kutia maanani
jinsi mgogoro wa mateka huko Iran ulivyomdhoofisha Rais Carter na jinsi
mgogoro wa mateka huko Lebanon ulivyokuja kumwathiri Rais Reagan katikati
ya miaka ya 1980.
Suala hilo lilipelekwa kwa Powell ambaye alifanikisha kuachiliwa kwa mateka hao
baada ya siku 11. Ulikuwa ni ushindi mkubwa lakini hata hivyo, Ikulu haikutaka
atokee kwenye televisheni kupata sifa alizostahili. Powell na Armitage walikuwa
wanataniana na kusema kwamba Powell alikuwa amewekwa katika kisanduku
cha barafu au kwenye friji ambapo alikuwa anatumiwa tu wakati akitakiwa.
Muda mfupi kabla ya mashambulizi ya September 11, jarida la times lilikuwa
limeandika habari moja kuu kuhusiana na Powell ikiwa na kichwa cha habari
“Umekwenda wapi Colin Powell”? Habari hiyo ilisema kwamba alikuwa
akiacha nyoyo zikiwa kwenye kina kirefu kuhusiana na sera mbali mbali na
kuonekana kuwa amemezwa na watu wenye msimamo mkali katika utawala
uliokuwa madarakani. Habari hiyo ilitoa changamoto kubwa kwa Ikulu ambako
maofisa kadhaa walikuwa wamewashikilia waandishi kuthibitisha kwamba
Powell alikuwa akifanya kazi kama kawaida wakati mwingine akiwa amekata
tama. Mara nyingi akifanya kazi kwa upweke akiwa amejikita pembeni na utawala
huo mpya.
Rove akiwa miongoni mwa maofisa hao alikuwa akisema chini chini kwamba
alikuwa anahisi Powell alikuwa ameteleza sehemu fulani na kwamba ilikuwa si
kawaida kumwona akiwa katika hali isiyoonyesha furaha akiwa na Rais.
31
TUNAINGIA VITANI.
Powell na watu wengine miongoni mwa washiriki wake walikuwa wametumia
masaa mengi na waandishi wa jarida la Times wakijaribu bila mafanikio
kuwajulisha kwamba habari waliyoandika haikuwa ya kweli. Lakini Powell na
Armitage walifahamu nguvu iliyokuwepo Washington ambako kuibuka na
kuanguka kwa umaafuru wa mtu ni jambo jepesi.
Tatizo lilikuwa kwamba msimamo huo wa habari hiyo ungeonekana kuwa
ndiyo ukweli hata kama haikuwa hivyo. Tatizo kubwa zaidi lilikuwa kwamba
habari hiyo kwa sehemu fulani ilikuwa ni kweli. Powell alikuwa haanzishi sera
mpya ya nchi za nje alikuwa akipangiwa majukumu ya kufanya na alikuwa
akikabili migogoro midogo mmoja bada ya mwingine. Lakini kama alivyowahi
kusema mara moja katika faragha, “ili kuweza kuendelea bila matatizo katika
ngazi za juu lazima uwe mjanja katika mchezo wako.”
Alipokuwa mwenyekiti wa jopo la Wakuu katika jeshi aliwahi kuandika baadhi
ya misemo aliyokuwa anaipenda zaidi na kuipenyeza chini ya kioo kilichokuwa
juu ya deski lake katika makao makuu ya Wizara ya Ulinzi. Moja ya misemo hiyo
ilikuwa “kamwe usiwaruhusu wakwambie kwamba unatapa tapa”.
Rais Bush alikuwa akiwahutubia wanafunzi katika shule ya Emma E. Booker
Elementary School huko Sarasota Florida wakati Rove alipomjulisha kwamba
ndege moja ilikuwa imeubamiza Mnara wa Kaskazini wa kituo cha biashara cha
kimataifa mwanzoni ilionekana kuwa tukio hilo lilikuwa ajali au labda kosa la
rubani ambaye huenda alikuwa na mshitulo wa moyo, Bush alifikiri.
Alikuwa amekaa kwenye stulu darasani akiwa amevaa suti yenye rangi nyeusi
shati la bluu na tai nyekundu, Ubao mdogo wa ukutani uliokuwa nyuma yake
ulikuwa na maandishi yasemayo “ Kusoma kunaifanya nchi istawi”.!
Andrew H. Card Jr mnadhimu wa Bush na msaidizi wa zamani wa Reagan na Bush
mkubwa aliingia na kumnong’oneza rais huyo moja kwa moja sikioni mwake
“ndege ya pili imeubamiza mnara wa pili, Marekani inashambuliwa”.
Picha ya hali iliyotokea wakati huo imebakia katika historia, mikono ya rais
huyo ilikuwa imekunjwa juu ya miguu yake wakati anageuka kusikiliza maneno
ya Card. Uso wake ukawa na sura tulivu kwa mbali japokuwa kulikuwa na
mshitukopamoja na kuchanganyikiwa.Bush anakumbuka vizuri kabisa
alivyokuwa, ‘nafikiri watu hawa wametangaza vita dhidi yetu, na nimeamua wakati
huu kwamba tunaingia vitani.” Alisema Bush.
Bush aliamua kwamba alihitaji kuwaeleza wananchi wake mambo kadhaa. Saa 3.30
asubuhi alitokea mbele ya kamera za televisheni katika kituo cha habari cha shule
hiyo ya Booker ili kutoa taarifa yenyewe. “kwa nini niliyarudia maneno hayo hayo
labda huo ulikuwa ni mwangwi wa matukio ya nyuma” rais huyu alisema
baadaye. “Sifahamu ni kwa nini nitakueleza ukweli kwamba hatukukaa kuyapanga
maneno haya. Nilisimama na kujikuta nikiyasema. “Mlichokiona ndiyo hasa mimi
mwenyewe nimeonyesha hulka yangu.”
32
Msururu wa magari ya rais huyo kwa kasi ulielekea kiwanja cha ndege cha
kimataifa cha Sarasota Bradenton. Alichepuka haraka akipanda ngazi na kuingia
katika chumba cha ofisi yake ya faragha ya ndege yake ya serikali ya Air Force
One. “hakikisheni mke wangu na mabinti zangu wanalindwa” hiyo ndiyo ilikuwa
amri yake ya kwanza kwa maofisa wa vyombo vya upelelezi. “Bwana Rais
alisema mmoja wa maofisahaokwa unyonge, “tunatakaukae haraka
iwezekanavyo.”Bush alikaa kitini na kujifunga mikanda na ndege ikaanza
kuondoka taratibu na muda si mrefu ikapaa angani kwa kasi.
Mke wa Rais huyo Laura Bush akiwa amevaa suti nyekundu na mikufu miwili ya
mapambo ya lulu shingoni mwake alikuwa katika chumba cha Caucus katika
jengo la Ofisi ya Seneti la Russe mjini Washingtoni akiwa tayari kutoa hoja
kuhusu watoto kuanza elimu mapema mbele ya kamati ya Seneta Robert M.
Kennedy mara wakapata habari kuhusu ajali hiyo na bibi Bush, Seneta Kennedy
na watu wengine wakaondoka kupitia mlango wa pembeni. Baada ya maelekezo
ya tukio hilo Bibi Bush alifanya juu chini kujituliza. Uso wake ulipauka mara
moja machozi yakimlenga na midomo yake ikitetemeka kwa woga.
Kisha makao makuu ya jeshi la Marekani yakashambuliwa, na wapelelezi na polisi
wa kamzingira. Walimweleza nia ya kumpeleka katika eneo lenye usalama. Kundi
hilo mara moja likaondoka haraka.
Saa 3.50 Bibi Bush alikuwa akisubiri watu wa kumsindikiza katika msongamano
wa magari kutoka jengo la bunge la Seneti (Capito), ilichukua dadika 45
kumfikisha kwenye makao makuu yake na alipelekwa katika chumba cha
Mikutano cha Wood. Saa 4.51 ndipo vyombo vya usalama vilipoamua Kend
kumficha katika Ofisi ya New Havana mtu mmoja aliyejuliakana kwa jina la
Turquoise ambalo lilikuwa jina la siri la Barbar Bush Bint wa rais huyo
aliyekuwa na umri wa miaka 19 akisoma huko . Twinkle jina jingine la siri la
binti mwingine pacha wa Rais Bush. Akiwa anasoma Chuo kikuu cha Texas huko
Austtin alipelekwa kufichwa katika Hotel ya Driskill dakika sita baadaye.
Ilikuwa saa 3.39 asubuhi ambapo ndege ya America Air lines Safari namba 77
aina ya Boeing 757 ilipobamizwa katika jengo la makao makuu ya jeshi la
Marekani. Dakika tano baadaye aliweza kuwasiliana kwa simu na makamu wake
wa rais Dick Cheney ambaye alikuwa amekimbizwa kutoka katika ofisi yake ya
upande wa magharibi na maofisa wa usalama na kupelekwa katika kituo cha
shughuli za Dharura cha Rais (Presidential Operations Center - POC) ambacho
ni handaki maalum la dharura lililo chini ya viwanja vya Ikulu.
33