The new chinese home made passenger jet

Emmanuel Alden

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2016
Posts
388
Reaction score
486
Kule China hii leo ndege yao ya kwanza ya abiria imefanyiwa majaribio ikiwa na abiria 70 je unadhani uthubutu wa China katika sekta ya anga itatingisha makampuni makubwa kama Boeing na Airbus pamoja na bombardier kutoka ulaya na marekani au Africa tu ndio watanunua ndege hizo maana ni cheap na jee itaweza kuyashawishi mashirika makubwa ya ndege kutoka ulaya na marekani lakini pia Asia, Mimi sijui tulijadili hili wadau.
 
China ina soko kubwa sana la ndani la ndege za ukubwa wa kati za kusafirisha abiria.Mashirika ya ndege ndani ya uchina yanategemea sana ndege za boeing muundo wa 737 na airbus muundo a320.Ndege waliyobuni wachina c919 inashindana na hiyo miundo ya boeing na airbus.

Na hiyo ndege yao c919 ikifanyiwa majaribio na kukidhi vigezo vyote vya urushaji ndege ya abiria, basi tena china itawaambia boeing na airbus bai-bai: hawataagiza ndege zao tena! Zipo pia nchi za asia ambazo zitapendelea kununua ndege toka china badala ya kutoka boeing au airbus au bombardier ya canada.

Kwa hiyo katika tasnia ya ndege za abiria boeing na airbus wanahofia ujio wa china kwenye uwanja!
 
Tumeumia waafrica
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…