Ndugu yangu, ni shida tu hapa bongo ni kuwa mtu anapopata nafasi ya kujiunga kanma academician, inabidi yeye mwenyewe apigane hadi aweze kupata hayo unayosema ndo maana wale watu ninaowaita smart guy wengi wao wakisha pata nafasi wanapotea kwanza, akija kurudi huku Tz ameshazeeka anatumika kidogo muda wake wa kuishi unaisha au kesha choka kufanya kazi kwa nguvu. kuna mizengwe mingi mno, ukiritimba mwingi lakini yote hayo hakuna kurudi nyuma, lazima tuelewe tuna jukumu kubwa la kuhakikisha watanzania wanaishi sawa na mtu aliye marekani kisayansi na technologia kwa kujitoa mhanga. Pia niseme tu wengi wa instructors vyuo vyetu vya elimu ya juu ni wale ambao hawana PhD holder, huko form six ni wale ambao ni diploma hoders na Form six leavers, form form ni wale mabao ni form six leavers na form form leavers, taasis husika zinatakiwa kuona hiyo hali na kuirekebisha haraka. Ni wimbo wa miaka sasa, sehemu nyeti hatuzitilii maanani, tunabaki kaufanya vitu vya leo na kesho hatuna uhakika tutafika au laa! Unaposikia tunaboresha secta ya uwekezaji, je tuko tayari hata kuiba technologia ya hao jamaa wanaokuja kutuibia mali ghafi au tunajipa moyo kuwa siku moja nasisi tutasimama kam watZ. Hayo namwachia JK na serikali yako, haswa wizara ya sayansi na technologia kuona na kuchukua hatua madhubuti ya kuwapa scholarship hawa intructors waende sehemu ambayo itawajenga kiuwezo kupata maarifa ya kuja kuwajuza watz wenzetu kwa manufaa ya baadae. Samahani kama kuna sehemu nimekwaa mtu.