Kama lugha ya yai inapanda, utamuelewa Ali Mfuruki, mimi nimemsoma huku nimetulia nimemuelewa sana. Kwanza ameunga mkono bomoa bomoa zote katika road reserve, open spaces, unplanned areas na risky buildings.
Amesema anatatizwa ule umbali wa mita 60 toka kwenye njia za maji, tangu DSM City Master Plan ya mwaka 1968-1979 haijatekelezwa, na Master plan mpya ya 2012-2032 ambayo mpaka sasa haijapitishwa na huu ni mwaka wa 6!, hakuna popote ufafanuzi hizi mita 60 ni kwenye njia zipi za maji?. Amesema kama sheria hiyo ingekuwepo, tusingekuwa na beach hotel hata moja!, amesisitiza anatatizo na tishio la kuwabomolea watu mahekali yao kule beach na kuuliza, kwa kuyabomoa, serikali inataka kupata nini?, ametolea mfano mji wa Amsterdam, usingekuwepo, akatolea mfano jiji la London na majijini mengine, mto unapita katikati ya mji na hakuna tatizo. Hoja yake ni waliojenga beach, wapewe jukumu la kujenga miundo mbunu rafiki ya kuhifadhi mazingira ya maeneo yao na kutolea mfano Kunduchi Beach, Bahari Beach na Africana hotels, au kitu kinachofanyika barabara ya Ocean Road.
Mimi sina nyumba beach area lakini naungana kabisa na logic ya Ali Mfuruki. unawabomea watu mahekalu yao ili uhifadhi nini, wakati hayo mahekalu yanaweza kuwepo na mazingira kulindwa!.
Paskali