TFF nini wajibu wenu kama mnashindwa kusaidia timu?

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,317
Mpira wa Afrika umejaa figisu bila miamala hauendi.
Juzi E Gine tumeshinda mbili kwa moja lakini ukiangalia penati ya Samata ilikuwa wazi kabisa Refa akatupotezea bila juhudi binafsi za wacheji huenda ingekuwa sare.

Jana na Libya tumenyimwa penati ya wazi kabisa halafu wao wamekuja kupewa penati ya mguuni mambo ya ajabu kabisa.

Ukiangalia mechi zote kwa jicho la tatu unaona kabisa Miamala imetumika dhidi yetu.

Refa wa kwanza alikuwa wa Burundi hapo Jirani tu ambao kila kitu wanategemea kwetu mlishindwa nini kukaa nae kabla?

Refa na Libya ni Mmalawi wote majirani mlishindwa nini kuweka mambo sawa?

Timu inacheza vizuri ila kamati ya ufundi imelala kabisa ni kama haipo.

Waarabu hawashindagi kihalali kuanzia ngazi ya vilabu hadi timu za Taifa, hata kama timu inakiwango kiasi gani lazima kamati za ufundi zihusike nje ya uwanja.

Kwa kweli tusipofuzu mwaka huu lawama zote Kwa TFF kwa uzembe wa wazi kabisa.

TFF tunahitaji point zote tisa pale Taifa, kila mmoja ashinde mechi zake kinyume na hapo mjiuzulu tu.!
 
Sijawahi kuona mtu mpumbavu kama mtanzania. Yeye anawaza kuweka mazingira ya rushwa hadi kwenye mambo ya msingi.
 
Sijawahi kuona mtu mpumbavu kama mtanzania. Yeye anawaza kuweka mazingira ya rushwa hadi kwenye mambo ya msingi.
Mnavyolalamika kuonewa na Marefa mnafikiri mnaonewaje, hii dunia haina usawa.. Mwenye nguvu ndio mshindi.
 
wawasilishe malalamiko pamoja na Video za ushahidi ili iwe mwisho kutuonea
Wapi wawasilishe sanasana watamwadhibu refa tu lakini point haturudishiwi, hiyo ndio inakuwa nitolee.
 
Sijawahi kuona mtu mpumbavu kama mtanzania. Yeye anawaza kuweka mazingira ya rushwa hadi kwenye mambo ya msingi.
Mpumbavu mtanzania anawaza rushwa
Ila unaeona sio mpumbavu anatekeleza
Rushwa alikua anachukua Blatter itakua hapa bongo mkuu mpira bila fitina hauendi Usione tu
 
Mpumbavu mtanzania anawaza rushwa
Ila unaeona sio mpumbavu anatekeleza
Rushwa alikua anachukua Blatter itakua hapa bongo mkuu mpira bila fitina hauendi Usione tu
Wabongo wengi wanakaririshwa, Duniani mambo haendi hivihivi bila mipango .

Hapa hapa Tanzania huwezi kupewa Tenda, kandarasi ama mkataba wowote bila 10%, hata kama unaenda kuokoa maisha ya maelfu ya watu.

Watu watakukazia tu.
 
Wapi wawasilishe sanasana watamwadhibu refa tu lakini point haturudishiwi, hiyo ndio inakuwa nitolee.
lakini pia unajisikiaje refa ametuibia wazi wazi halafu asichukuliwe hatua? hatuwezi kurejeshewa point ila hizi tabia zikome ndo zinakwamisha maendeleo ya mpira Africa fikiria kwa upana zaidi
 
Back
Top Bottom