TFF NA BIASHARA YA MPIRA

babi

Member
Jul 24, 2012
79
109
Ligi Daraja la Kwanza ndio hiyo inaelekea Ukingoni huku leo kukiwa na Michezo kadhaa ya kukamilisha Ligi hiyo. Michezo hiyo itaamua ni nani anapanda na nani anabaki na yupi anashuka. Wacha nizungumzie kundi C ambalo lipo katika Vita kubwa kati ya Timu mbili Geita Gold Mine na Polisi Tabora ambazo Mpaka Jana asubuhi zilikua na Point sawa katika Msimamo kila mmoja na Point 27 huku wakiwa na mchezo mmoja Mkononi. Tofauti ni Goli moja ambalo Polisi Tabora Wamewazidi Geita Gold. Katika Mchakato wa Ligi Timu ya Panone fc ambayo ipo katika Kundi C iliweza ikatia Rufaa Timu ya Polisi Tabora kwa kuchezesha wachezaji ambao si Raia na hawakufuata utaratibu. Kwa jinsi matokeo ya Rufaa ile yangeweza kuamuliwa kwa wakati Timu ya Panone fc ingeweza kuwa na Matumaini na kuongeza Ushindani ya Kupanda ligi Kuu. Lakini Majibu ya Rufaa yale kutolewa Mapema yangeathiri Malengo ya Viongozi wachache wanaoibeba Timu ya Geita Gold ambayo imeanza ligi ikiwa na Kiasi cha milioni mia tatu Mkononi kwa ajili ya kupandisha Timu kwenda Ligi kuu. Rufaa ilihairishwa kwa sababu zisizo na Msingi na timu ya Panone fc kupata taarifa kuwa watapewa majibu ya Rufaa yao. Baada ya Kuona Polisi Tabora watacheza Mechi ya Mwisho na Timu ya Jkt Oljoro ambayo ni timu ya Jeshi la Wananchi na Polisi Tabora ni timu ya Jeshi la Polisi huku Geita wakicheza na Kanembwa ambayo ni timu ya Jeshi la Wananchi. Kiufupi timu hizi tatu Kanembwa, Oljoro, Polisi Tabora ni Timu za Taasisi zinazosikilizana. Viongozi hao wanaoua Mpira wa Tanzania wakaona wawatafutie Geita Point za Mezani na Jana Geita wamepewa point tatu za Mchezo wao waliocheza na Oljoro ambao ilivunjika. Point tatu hizo zinaifikisha Geita Point 30. Ili Polisi Tabora iweze kufuzu inahitsji ushindi na Goli nyingi ili kuweza kufikia Point 30 na timu ya Geita inahitaji kupoteza Mchezo ili iweze kubaki.

Sasa matokeo yakiwa hivyo Viongozi hawa wanaofanya Biashara ya Mpira ambao Tayari wameweka kibindoni Mgao wao watakuja na Maamuzi hayo ili tu kuipandisha Geita. Maamuzi ni kuinyang'anya Polisi Tabora Point 5 na kuipa Panone fc Point ambazo hazina faida kwa wakati huu kwa timu ya Panone Baada ya kuihujumu katika kuikosesha nafasi kwa makusudi.

Kila jambo Lina Muda na Muda wa yote unafika. Ifike wakati sasa Serikali iingilie kati kunusuru Soka la Tanzania na kuondoa wafanyabiashara wa Mpira pale Tff. Bila hivyo tutaendelea kuifanya timu ya Taifa kama Mradi wa watu wachache huku wachezaji wakiwa ni walewale tuliowazoea na vipaji vilivyo huku chini kwenye ligi daraja la kwanza na la pili vikifukiwa na watu wachache wanaoangalia Naslahi yao.

#PAZA SAUTI KWA SOKA LA TANZANIA
 
..nimesikia mmoja kashinda saba na mwingine kashinda nane!!
very funny indeed!
 
Back
Top Bottom