Binafsi sioni upendeleo wowote zaidi ya ushamba wa Kuendesha soka. Huwezi kuwa na viongozi wasio na maono ukategemea maendeleo.TFF timu pekee wanayoijali ni SIMBA. hizo nyingine sijui LIPULI hawana habari nazo. usishangae rais wa tff atahudhuria mechi ya kuwakaedhi simba kombe kesho lakin hiyo fainali huko lindi hatakuja! hii ndio tff
Lipuli wana hoja hapa! Ila kwa namna wanavyotukamiaga acha wateseke! Wametuharibia sana msimu huu!Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) mnapaswa kuionea huruma Lipuli Fc, timu hii inashiriki mashindano mawili yaani Ligi kuu na shirikisho lakini mara nyingi ratiba inazokutana nazo ni kama vile haya mashindano yanasimamiwa na vitu viwili tofauti na si TFF.
Mara ya kwanza makosa haya yalionekana mchezo wa nusu Fainali ambapo Lipuli ratiba ilionyesha anatakiwa aende mkoa wa Mara tarehe 3/5/2019 kisha Arudi Iringa kupambana na Yanga nusu fainali tarehe 6/5/2019 ambapo ni dhahili kabisa kwa uwezo wa club hii wasingeweza, lakini nadhani Lipuli waliomba basi angalau mchezo na Biashara Urudishwe Nyuma hadi tarehe 30/4/2019, wakati Lipuli inatoka Mkoani Mara mshindani wake Yanga alikuwa anatoka Mkoa wa mbeya tu ambapo ni masaa matano au sita kufika Iringa..hapo utaona nani anapata faida. Lipuli kabla ya kucheza na biashara Ilikaa wiki tatu bila kucheza hata Biashara nao hawakuwa na Mchezo wowote kwa muda mrefu ambapo kwa busara za TFF kama zingetumika na ukiangalia umuhimu wa nusu fainali ile basi mchezo ule ungepangwa mapema kabisa ili kuzipa timu shiriki muda wa kujiandaa.
Hayo yalikuwa ya nusu Fainali , sasa imekuja hii ya fainali yenyewe, kwa kawaida fainali ni jina kubwa na lenye hadhi, ukisikia fainali hata maandalizi yake lazima yawe makubwa, lakini kwa TFF fainali ya shirikisho haipewi umuhimu huo, Faibali timu zinatakiwa zipewe muda wa kujiandaa ili kuleta msisimuko na hadhi ya shirikisho lakini tofauti kabisa na fainali za shirikisho mwaka huu. Fainali za mwaka huu zitapigwa uwanja wa Ilulu mkoani Lindi na zitavikutanisha vilabu viwili vya Azam na Lipuli. Fainali hizi zitachezwa tarwhe 1/6/2019, hapa ndipo penye shida.
Michezo ya kumaliza ligi inachezwa tarwhe 28/5/2019 huku Azam akiwa mkoani Dar es Salaam na Lipuli atakuwa anakwaana na Prison mkoani mbeya, AZam atatumia masaa sita au saba huku Lipuli wakitumia zaidi ya masaa 18 kufika Lindi, hii inamaanisha Lipuli wamalize tarehe 28 kisha waondoke wakacheze tarehe 1 mwezi wa sita, ambapo kwa vyovyote file timu itafika tarehe 30 lindi kisha tarehe moja acheze mechi ya Fainali...hiki ni kituko na ni dhuruma kubwa kwa Lipuli, Azam yeye atafika huenda tarehe 28 usiku au tarehe 29 na atapata muda mzuri wa kujiandaa kuliko Lipuli ambayo haitapata huo muda.
Kwa vyovyote vile TFF muangalie namna gani Lipuli itapata ahueni na muda wa kujiandaa na hiyo mechi, Muifanye fainali hii iwe ya ushindani na yenye mvuto, kuliko kuacha ratiba hii ambayo ni dhahiri itaibeba AZAM
Wacha dawa iwaingie kitu walichotufanyia msimu huu ni halali kwa wanayowakuta,wao wabajua kuikamia yanga tu basi!Lipuli wana hoja hapa! Ila kwa namna wanavyotukamiaga acha wateseke! Wametuharibia sana msimu huu!
Simba wapi???...hao waliokuwa wanapumzika siku moja alafu kesho yake wanacheza mechi....simba anacheza tarehe 19 dar es salaam alafu tarehe 21 anamechi singida...hayo yote watu hawayaoni but kwa kuwa ni mashabiki wa yanga wamebakia kulia lia tu huku mitandaoni na kulalamika kuwa simba anabebwaTFF timu pekee wanayoijali ni SIMBA. hizo nyingine sijui LIPULI hawana habari nazo. usishangae rais wa tff atahudhuria mechi ya kuwakaedhi simba kombe kesho lakin hiyo fainali huko lindi hatakuja! hii ndio tff
Sio kuikamia yanga tu...timu zote za ligi kuu zinapokutana na simba or yanga huwa zinakamia...na kufungwa kwenye mpira ni kawaida hata ukimleta barcelona aje acheze kwenye ligi yetu ingawa uhakika wa kuchukua ubingwa ni 100% but kuna mechi lazima atafungwa tuWacha dawa iwaingie kitu walichotufanyia msimu huu ni halali kwa wanayowakuta,wao wabajua kuikamia yanga tu basi!
Binafsi sioni upendeleo wowote zaidi ya ushamba wa Kuendesha soka. Huwezi kuwa na viongozi wasio na maono ukategemea maendeleo.
1.Timu inakaaje wiki 3 bila mechi utafikiri ligi imesimama kupisha majira ya baridi?
2.Timu itapewaje mapumziko wiki 3 bila mechi kisa inashiriki maahindano ya kimataifa?
3.Uliwahi kuona ligi gani duniani (Hata Ndondo) timu inakuwa na mechi 13 viporo?
4.Ni kawaida mechi ya ligi kuahirishwa timu ngeni imeshaondoka iko njiani.
5.Ratiba ya ligi inapangwa kwa kufuata "siasa" za Simba & Yanga.
6.Mchezaji aliyefanya kosa anaahirishiwa kutekeleza adhabu hadi mechi ya Simba na Yanga ipite ndo aanze.
Binafsi naona ushamba zaidi ya upendeleo. Usishangae mwakani Yanga akawa na Viporo kama vya Simba mwaka huu ili kubalance mzani.
Namba sita imechekesha na kunionyesha bado tunasafari ndefu sana, Ila mwisho umekubali kuwa ukiacha ushamba wa viongozi bado kuna timu mbili zinapendelewa sanaBinafsi sioni upendeleo wowote zaidi ya ushamba wa Kuendesha soka. Huwezi kuwa na viongozi wasio na maono ukategemea maendeleo.
1.Timu inakaaje wiki 3 bila mechi utafikiri ligi imesimama kupisha majira ya baridi?
2.Timu itapewaje mapumziko wiki 3 bila mechi kisa inashiriki maahindano ya kimataifa?
3.Uliwahi kuona ligi gani duniani (Hata Ndondo) timu inakuwa na mechi 13 viporo?
4.Ni kawaida mechi ya ligi kuahirishwa timu ngeni imeshaondoka iko njiani.
5.Ratiba ya ligi inapangwa kwa kufuata "siasa" za Simba & Yanga.
6.Mchezaji aliyefanya kosa anaahirishiwa kutekeleza adhabu hadi mechi ya Simba na Yanga ipite ndo aanze.
Binafsi naona ushamba zaidi ya upendeleo. Usishangae mwakani Yanga akawa na Viporo kama vya Simba mwaka huu ili kubalance mzani.