Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,052
- 7,609
Nchi yetu ina tatizo la watawala na viongozi kufanya mambo ya maendeleo kwa njia ya kujitoa na kusakiziana badala ya kuungana (teamly) kuyatatua matatizo ya watu. Na kuvutana huwa hakusaidii kufumbua tatizo lakini kumuunga mwenzio mkono hata kama kweli wewe hilo jambo hausiki haiwezi kuonekana eti ni fedhea kwako.
Binafsi sijuhi nani haswa anahusika katika kuhakikisha majukwaa ya maana yanawekwa pale Kaitaba lakini kuendelea kuuacha ule uwanja jinsi ulivyo huku watizamaji wakiishia kukaa kwenye majani kama nyoka na wengine wakining'inia kwenye miti kama "sokwe" ni aibu kubwa sana kwa waendeshaji wa masuala ya mpira wa miguu.
Mie naamini kabisa kwamba mlipoamua kuweka carpet pale, mlilenga kuufanya uwanja kwa ujumla huwe wa kuvutia, sasa huu ni mvuto gani kama 75% ya watizamaji wamekaa chini na kupanda mitini mithiri ya nyani? kusema kweli ni vihoja na unaleta kinyaa
Yawezekana KRFA ndo wanahusika, yawezekana Malinzi ama Tff kwa ujumla ndo inahusika ama ata manispaa. Ni kwanini hamjengi utaratibu wa kubebana kwenye mambo ambayo kimsingi ni kwa manufaa yenu nyote? Ugumu wa kutenda kama timu uwanjani mnaupata wapi, na kama nyinyi hamuwezi kuongoza kama timu ni vipi sasa mtaweza kuziongoza timu zisalie kuwa timu na si vipande?
Kuliko kuujengea vile na mwisho mkajiweka kando ni mara mia mngeuacha vile vile na badala yake hizo nyasi zikapelekwa kwenye viwanja vyenye majukwaa tayari kama Kambarage (Shy), Sokoine (Mby), Jamhuri (Dom) n.k. Huu ni upuuzi mkubwa kweli kweli.