Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,490
- 96,054
Nikiwa ni mdau wa soka la Tanzania nimesikitishwa sana na vitendo vya washabiki wa timu haswa ya coast union ya tanga vilivyo jitokeza katika mechi ya coast na yanga, kitendo cha kuwashambulia wachezaji kwa mawe wakiwa uwanjani siyo cha kiungwana kabisa hata kama walikwazwa na maamuzi ya waamuzi, wachezaji hawakutakiwa kuhukumiwa hata kidogo na walichotakiwa ni kuwahimiza viongozi wao kufuata sheria zinazo ongoza soka hapa nchini.hii ni mara ya pili tukio la washabiki wa timu hiyo kufanya uhuni huo.Tuna iomba Tff kupitia kwa rais wake Jamal Malinzi kukomesha hiyo tabia chafu.