muda wa ukombozi
Senior Member
- Jun 28, 2013
- 129
- 118
TFF KATOA!! KACHUKUA!! JE ATATOA TENA?
Tff ndio chombo chenye dhamana wa mpira wa miguu kwa hapa Tanzania, wao ndio wanatunga sheria, kanuni na adhabu pale ambapo sheria na kanuni zimekiukwa.
Tff ndio taasisi ambayo inapaswa kuwa na kumbukumbu ya matukio mbalimbali yanayotokea uwanjani kwasababu wao ndio wanaowamiliki waamuzi na makamisaa wa kila mchezo na kama vile haitoshi, waamuzi na makamisaa taarifa yote ya mechi wanaipeleka tff kwa ajili ya kumbukumbu.
Kwa hapa kwetu kumbukumbu za taarifa ukiacha tff unaweza ukazipata Azam Televisheni lakini ili uzipate habari hizi lazima tff watoe ridhaa au kwa mujibu wa mkataba wao walioingia kuonesha au kuweka kwenye kumbukumbu mechi zote za ligi kuu na zile za shirikisho.
Lakini na klabu pia inakuwa na kumbukumbu za mechi pamoja taarifa mbalimbali kuhusu wachezaji wao na timu kwa ujumla.
Nikiwa nipo maeneo ya mbagala kwenye vijiwe mbalimbali vya wafuatilia soka nimegundua kuna majonzi na furaha kwa maamuzi yanayotolewa na tff, kwenye kila maamuzi yanayotolewa yanakuwa na mashabiki wake, kwasababu kunakuwa na faida kwa upande wa timu fulani na hasara kwa upande wa timu nyingine, lakini nimekuja kugundua hata kwa wale wanaotoa maamuzi hayo kuna kuwa na faida kwao kwasababu ya unasaba wa ushabiki wao na timu fulani, asikuambie mtu ushabiki kitu kibaya sana, watu wanakufa kwasababu ya ushabiki,kuna watu wanapigana mtaani kwa kubishana tu nani mkali kati ya Messi na Ronaldo, kuna mashabiki wanazimia uwanjani tunaona pale uwanja wa Taifa timu zao zikiwa taabani, hayo machache tu, narudia tena asikuambie mtu ushabiki sio mchezo na bahati mbaya sana kama umezaliwa Tanzania miaka ya 90 kwenda chini na nimpenda mpira lazima utadondokea kati ya Simba au Yanga naomba usiniulize mimi timu gani tafadhali!!!
Kuna madai yapo na yanaendela kutamalaki kwenye viunga mbalimbali na vijiwe vya mpira kwamba ile kamati ya masaa 72 ilikuwa imejaa wajumbe wengi toka klabu ya simba, na hii na tuhuma hizo zilienezwa na kiongozi mmoja wa kalabu ya Yanga (Salum Mkemi) huyu kiongozi alionekana shujaa kwa kusema ukweli, ikaonekana mbele ya mashabiki yale maamuzi ya kupewa pointi 3 na magoli 3 klabu ya simba kutoka kwa Timu ya Kagera kwa kumchezesha Mohamed Fakhi ambaye alikuwa ana kadi tatu za njano ambayo yalikuwa faida kwa Klabu ya Simba, maamuzi hayo yalikuwa na unazi na unasaba na ushabiki wa simba.
Maamuzi hayo yalikatiwa rufaa, kikubwa ambacho mashabiki wengi tulikuwa tunajua rufaa ilikuwa inahusu Mohamed Fakhi kutokuwa na kadi tatu za njano lakini wakati rufaa hiyo ipo kwenye mchakato wa kusikilizwa akatokea kiongozi wa Simba naye akaituhumu kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kuwa inahusisha viongozi wenye ushabiki na unasaba na Yanga, hiyo kamati kwanza ikampa adhabu huyo kiongozi wa simba (Haji Manara) aliyeituhumu na kama vile haitoshi zile pointi zikachukuliwa na kurudishiwa Kagera Sugar.
Kikubwa ambacho wapenda soka wangetaka kujua, rufaa hiyo ilikatwa na kagera sugar au viongozi wa tff??
Hizo adidu za kukata rufaa zilikuwa zinaongelea rufaa kukatwa nje ya muda, zinaongelea simba kutolipa ada ya rufaa?
Viongozi wa Kagera sugar walijua simba haijalipa ada ya rufaa na walichelewa kukata rufaa husika, kwasbabu kilichokuwa kinaongelewa ni uhalali wa Mohamed Fakhi kuwa na kadi tatu za njano au la! Masuala ya uhalali wa simba kukata rufaa au kutolipa ada ya rufaa hatua hiyo simba ilishavuka pale ambapo rufaa ilikubalika na kamati ikakaa na maamuzi yakatolewa.
Ninavyojua mimi, rufaa lazima ikatwe kulingana na maamuzi yalivyoamuliwa , rufaa ya kagera ilikuwa ni kupinga kuwa mchezaji wao hana kadi tatu za njano na walikuwa wanatoa povu kwelikweli kuwa hana kadi ya njano, maamuzi ya kamati yanakuja na madai ya kuwa ile kamati ya masaa 72 ilikuwa haina mamlaka ya kusikiliza rufaa ya simba kwa sababu rufaa ilikuwa haina uhalali wa kusikilizwa na tff, kwa sababu ilikuwa haijalipiwa ada na pia ilikatwa nje ya muda kwahiyo hapakuwa na rufaa ya simba tff kwa mujibu wa kanuni na sheria za tff.
Je rufaa ambayo haina uhalali inahitajika ijulikane wakati gani, pale ambapo rufaa inaletwa kwa mara ya kwanza kwa ajili ya uhakiki na kusajiliwa tff au kuna kamati ndogo inakaa kuhakiki uhalali wa rufaa husika mbona rufaa ya Polisi Dar haikuwa kama hivi?
kwenye kombe la FA Polisi Dar walikata rufaa kwa simba kumchezesha Lufunga akiwa na kadi tatu za njano ile rufaa ilitupiliwa mbali mapema kwasababu walikata rufaa nje ya muda na hawakulipia ada ya rufaa. kwanini isingetokea hivi kwa simba?
Je swali la kujiuliza ni kweli Simba ilikata rufaa nje ya muda? Je simba ni kweli ilikuwa haikulipia ada?
Yasije yakatokea yale ya simba na coastal union mara pointi tatu zinatolewa kwa timu husika!! Baada ya siku kadhaa zinachukuliwa!! Baada ya siku kadhaa zinatolewa tena kwa timu husika.
Hii inatuaminisha tff inakuwa inapanga nani awe bingwa kama wakiona pointi husika zinaweza kuwa na faida kwa timu ambayo hawataki iwe bingwa inaweka figisu, baadae wakiona ata wakipewa pointi hazina faida, hawawezi kuchukua ubingwa, zinarudishwa!!
Tuache kutoa maamuzi tukiwa na migongano ya kimaslahi na tuache kupeana uongozi kwa ukabila, tuangalie uweledi wa mtu, hii nchi ni ya watanzania msiwekane na makarundikana hadi tusioona tukajua!!
Ushabiki noma.

Muda wa ukombozi