TFF iweke marufuku kwa viongozi wa mpira kuzungumzia mambo ya TFF pia kukosoa maamuzi ya refa

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Pole Mtani nasikia nawakwenu naye kala Ban.

Ningependa kuishauri Tff ipitishe sheria kali kuzuia viongozi wote wa mpira hasa wasemaji wa vilabu vyetu kuacha kuzungumzia mambo ya tff na pia kukosoa maamuzi ya refarii.

Umakuta kiongozi wa mpira baada ya kuzungumzia mambo ya Klabu yake anaanza kuzungumzia mambo ya Tff wakati klabu yake ina matatizo chungu mzima.

Najua Tff ina raisi wake mpaka msemaji wake hakuna maana ya viongozi hawa wengine kuanza kuzungumzia mambo ya Tff

lingine ni Kuhusu marefa unakuta wasemaji wa vilabu wanawazungumzia marefa kama wanavyota na lugha chafu juu.

Ila hapa Tff mmevidekeza hivi Vilabu yani refa anapangwa kuchezesha mechi halafu timu zinamkataa na nyie mnakubali sijawai kuona.

Pale Uingereza hakuna kocha mwenye ruhusa na kukosoa maamuzi ya Refa tumeona makocha wakila mvua za kutosha kisha kukosoa maamuzi ya marefa.
 
Back
Top Bottom