TFDA yakamata shehena kubwa ya vipodozi vilivyopigwa marufuku Dar

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais na Jeshi la Polisi, imefanyaukaguzi maalum na kufanikiwa kukamata shehena kubwa ya vipodozi vilivyopigwa marufuku na Serikali katika baadhi ya majengo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na thamani yake haijajulikana mara moja haditathmini ikakapokamilika.

Akiongea na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti B. Sillo ambaye alikuwa nimiongoni mwa washiriki wa zoezi hilo kwa masikitiko makubwa, alisema “ Kiasi cha vipodozi hivihatarishi vyenye madhara kwa watumiaji na ambavyo vimeshapigwa marufuku na Serikali, ni kikubwakatika historia ya ukaguzi hapa nchini na wafanyabiashara wote wanaohusika na biashara hii haramu ni lazima wachukuliwe hatua stahiki za kisheria”.

Mkurugenzi Mkuu huyo, aliendelea kusema kwamba kwa vile vipodozi hivi huingizwa kwa njia yamagendo, ukaguzi huo ni endelevu na wahusika hawataweza kukwepa mkono mrefu wa Serikali mahalipopote na wakati wowote.

Alitoa rai kwa wafanyabiashara kuacha mara moja kuvunja Sheria za nchi na wasalimishe kwa hiyari yao vipodozi vyote vilivyopigwa marufuku TFFDA badala ya kusubiri Taasisi hiyo iwafuate.Katika hatuanyingine, Mkurugenzi Mkuu huyo aliwaasa wananchi kufanya maamuzi sahihi ya kutumia vipodozisalama vilivyosajiliwa na Mamlaka na kuachana na vile vilivyopigwa marufuku ili kulinda afya zao.

Zoezi hili limefanyika kuanzia tarehe 21/4/2016 na haikuelezwa mara moja kwamba litaisha lini
5.JPG
 
Back
Top Bottom