TFDA tusameheni-mtatuua walalahoi!

rakeyescarl

JF-Expert Member
Dec 9, 2007
481
145
Wadau.

Nimeshangazwa sana hi hatua ya TFDA kutoza gharama katika kuhakiki dawa. Nimekuwa nikitafuta vidonge nilivyoandikiwa na vinavyonisaidia bila kufanikiwa.

Nikapata mwana JF 1 akanitumia hivyo vidonge na kwa bahati akaweka Prescription niliyomtumia na yenye jina langu na kuandika kuwa ni for personal use. TRA wakaviacha,kufika kwa TFDA wananitoza pesa.

Nafikiri wangefikiria kusamehe kwa sababu hainiingia kichwani, vidonge hivi havipo na mgonjwa nimepata msaada na unanitoza wakati unajua kuwa mimi naumwa na kama sina uwezo wa kuvilipia hapo kwao basi ndio nikafe?*?

Nimeshindwa kuelewa!
 
Back
Top Bottom