Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,581
Mambo zenu!
Awali ya yote naomba nimshukuru sana Mh Rais kwa kutambua uwepo wa wasomi nchi hii, hasa 1st degree, Masters, PhD ,Proffesors na hata wale wenzetu wa fani ya Uhandisi (Engineering).Kwakweli nitakuwa mchoyo wa fadhira kama sitamshukuru Mh Rais.
Ukijaribu kuangalia, karibu kila idara, kila kitengo Mh Rais amejaribu kuwakumbuka wasomi sana. Anza tu na Baraza lake tamu la Mawaziri (Engineer, Dk & Proffesors).
Hali kadharika, makatibu wakuu, manaibu wakatibu wakuu, wakuu wa idara/vitengo na hata wakurugenzi wa mashirika ya umma, kwa kweli wengi(kama si wote), ni wasomi kabisa.Na ni mwaka wa kwanza na nusu toka aingie madarakani.
Kwa upande wa makada, wale ambao wamesoma kidogo kama mwenzangu DAUDI BASHITE, wameramba mashavu sana kwenye nafasi za Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, MaDC, maRAS, nafasi mbalimbali kwenye chama nk.
Naukumbuka usemi wa Mh Rais kwamba, maendeleo hayana chama.Na hii anaionesha kwa vitendo kabisa.Watu tofauti hata wasiokuwa wa CCM, Mh Rais anawapa nafasi mbalimbali za uongozi.Mfano Prof Kitila Mkumbo wa UDSM.
Huko nyuma, wasomi walianza kulalamika, kusononeka, kufadhaika , kuchanganyikiwa na kuwa na stress lakini sasa mambo yananoga.Rais hana hila na msomi.Anatupenda sote.
Mantiki ya kwamba anachukua wasomi vyuoni haina mashiko.Kwan hakuna vijana wengine mpk hao waendelee kukalia hayo maofisi?Tuache nongwa.
Asanteni sana