Tetesi za usajili kutoka klabu mbalimbali za Ulaya zikiwemo
Chelsea, Arsenal, Liverpool, Man City, Man United, Barcelona, Real Madrid n.k leo Jumapili 07/04/2019..........
Chelsea inahitaji pesa kiasi cha £100m kutoka
Real Madrid kwa ajili ya kiungo wa Ubelgiji Eden Hazard, 28.
(Independent)
Blues wamewasiliana na wakala wa mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski, 30.
Chelsea pia inamuhitaji mshambuliaji wa
Borussia Dortmund na Sweden Alexander Isak, mwenye umri wa miaka 19.
(Mirror)
Liverpool itaingia kwenye mbio za kuwania kumsajili mshambuliaji wa
Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 25, ikiwa mchezaji wao wa Senegal Sadio Mane, mwenye umri wa miaka 26, ataondoka Anfield msimu huu.
(L'Equipe, via Mail)
Mshambuliaji wa
Paris St-Germain Neymar, mwenye umri wa miaka 27, "Anajuta sana kuondoka
Barcelona," amesema mchezaji mwenzake wa zamani wa Barca na Brazil Adriano.
(Cadena Ser)
Manchester United imekuwa ikimchunguza beki wa kulia wa
PSG na Ubelgiji Thomas Meunier, 27, tangu mwanzoni mwa msimu huu.
(Sun)
Kiungo wa
Lyon Tanguy Ndombele anatakiwa na
Manchester United, lakini klabu hiyo ya England inakabiliwa na
PSG katika ushindani wa kuwania saini ya Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22.
(L'Equipe - in French)
Winga mkongwe wa
Bayern Munich na Uholanzi Arjen Robben, 35, ana uwezekano mkubwa wa kukataa mpango wa kujiunga na
nter Milan ili kuhamia ligi kuu ya Marekani MLS.
(Calciomercato)
Everton watapata £5m endapo mshambuliaji wao wa zamani Romelu Lukaku ataondoka
Manchester United mwishoni mwa msimu huu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ubelgiji anatakiwa na
Inter Milan.
(Telegraph)
Meneja wa
Newcastle Rafa Benitez amesema bado hajakaribia hata kidogo kutatua hatima yake ya baadae ndani ya St James' Park.
(Sky Sports)
Meneja wa
Bournemouth Eddie Howe amesema winga wa o raia wa Scotland Ryan Fraser ana uwezekano mkubwa wa kutokuwepo kwenye klabu hiyo msimu ujao. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 anawindwa na
Arsenal.
(Sun)
QPR wamefanya mawasiliano na Rui Almeida, meneja wa klabu ya
Troyes inayoshiriki league 2 nchini Ureno, ikiwa ni katika harakati za kutafuta mrithi wa Steve McClaren.
(Football.London)
Mtoto wa nyota wa soka wa zamani wa Brazil Ronaldinho amesaini mkataba wa miaka mitano na klabu ya
Cruzeiro. Joao Mendes mwenye umri wa miaka 14 amekuwa na klabu hiyo ya nchini Brazil tangu mwaka jana.
(Cruzeiro - in Portuguese)
CHANZO: Mtandao wa Castiradar