Katika hali isiyo tarajiwa na wengi ni kuwa wachezaji wa timu ya Dar es salaam Young Africa wamedokeza kuwa hawatakuwa tayari kuingia uwanjani katika mechi yao dhidi ya Mtibwa siku ya jumapili hadi hapo watakapolipwa malimbikizo ya mshahara wao wa miezi takribani mitano.
Mmoja wa wachezaji akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina amesema kuwa "hapo awali tulipo goma kufanya mazoezi uongozi ulituahidi kuwa utashughulikia matatizo yetu hivyo kutuomba radhi na kutupooza kwa fedha chache ambapo walitueleza kuwa hyo ni nje ya mishahara lakini cha kushangaza kadri siku zinavyokwenda hatuoni hatua zozote zikichukuliwa.
Awali ilkuwa tugomee mechi na Simba lakini uongozi ukatuahidi kuwa kwakuwa mechi hyo ina mapato mengi hvyo wangeyatumia kutulipa malimbikizo yetu lakini haikuwa hvyo hadi leo, yaani sisi wachezaji tunanuka dhiki kama siyo wafanya kazi wao.
Mchezaji huyo alienda mbali zaidi kwa kudai kuwa mwenzao(BOSOO) alivyogoma uongozi ulishtuka na kulifanyia kazi fasta tatizo lake iweje wengine.