The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Kuwa na mpango mkakati (strategic plan) katika biashara/kampuni yako ni jambo la msingi sana, hii hupelekea ufanisi na uhai mrefu wa biashara yako. Kwa mfano, katika makampuni 100 yenye mafanikio yaliyoorodheshwa na jarida la Forbes mwaka 1917 (Forbes 100) ni makapuni 3 tu yameweza kubaki sokoni mpaka dakika hii, hii ni kutokana na kuwa na mipango mkakati ambayo imeiwezesha makampuni haya kukabiliana na changamoto za kimasoko.
Tafiti pia zinaonyesha kwamba kampuni zinazojiendesha kimpango mkakati hufanya vizuri sokoni kuliko zile zisizojiendesha kimpango mkakati, hii hutokana na ubadilikaji wa mazingira katika soko pia ushindani katika biashara; ambao huongezeka kadiri siku zinavyozidi kwenda. Bain&Company mwaka 2007 walifanya mahojiano na watendaji wakuu 1,221 wa makampuni (global executives), 88% ya waliohojiwa walikiri kutumia na kutegemea mipango mkakati kama silaha (tool) katika uendeshaji wa kampuni zao.
Uandaaji wa mpango mkakati wa kampuni/biashara huweza kufanywa kwa njia (models) mbalimbali, lakini njia maarufu ni hii yenye kujumuisha hatua 4 zifuatazo;
- Kufanya uangalifu yakinifu wa mazingira (environmental scanning) hapa unapaswa kufanya ufuatiliaji (monitoring) na utathmini (evaluation) wa visababishi (factors) vyenye kuathiri utendaji wa kampuni yako (internal factors), ambavyo hujumuisha; rasilimali, utamaduni wa kampuni, miundombinu n.k. Kisha utaangali visababishi vipatikanavyo nje ya kampuni yako vyenye kuathiri utendaji wa kampuni yako (external factors) ambavyo hujumuisha; washindani wako, hali ya kiuchumi, taratibu za kisheria, hali ya soko n.k. Kimsingi hali zote hizi huathiri ufanisi wa kampuni yako. Njia maarufu itumikayo kufanya zoezi hili huitwa SWOC/T Analysis
- Uundaji wa mkakati (Srategic formulation), hapa utapaswa kuanza na kauli ya utume ya kampuni yako (mission statement), hii kauli itapaswa kuonyesha ni nini kampuni yako inafanya sasa (What's your organization now?). Baada kuwa na kauli ya utume, utapaswa kutengeneza malengo mahsusi (specific objectives), malengo haya yawe yametokana na (strategic issues) ulizoibua katika mchakato wa kwanza wa uangalifu yakinifu wa mazingira. Malengo yako mahsusi yanaweza yakagusa maeneo kama; ukuaji katika soko(market share/leadership), uongezekaji wa faida (profitability), ukuzaji wa hadhi ya kampuni (reputation), wajibu wa kampuni kwa jamii (taxes paid, participating in charities) n.k. Baada ya kuwa umetengeneza malengo yako; utapaswa kutengeneza mbinu (strategies) za kufikia hayo malengo (Utengenezaji wa mbinu utategemea na ngazi katika kampuni; ambazo ni corporate level, business level na functional level, hivyo kutapaswa kuwe na corporate strategy, business strategy na functional strategy). Baada ya kuwa na mbinu za kufikia malengo; utapaswa kutengeneza sera (policies) ambazo zitawaongoza wafanyakazi wa kampuni yako katika majukumu yao ili utekelezaji wa majukumu hayo umepelekee kufikia malengo ya mpango mkakati.
- Utekelezaji wa mpango mkakati (Strategy implementation),mpango mkakati hutekelezwa kwa kutumia njia (tools) mbalimbali ambazo hujumuisha; programs/projects, malengo makubwa (overall objectives/goals) ya programs/projects hizi yatapaswa kurandana na malengo mahsusi ya mpango mkakati kama tulivyoyaona hapo juu. Pia bajeti ya kampuni hutumiwa kama chombo cha kutekelezea mpango mkakati wako.
- Tathmini na udhibiti (Evaluation and control) hapa utapaswa kufanya ulinganifu kati ya matokeo baada ya utekelezaji wa mpango na malengo yaliyowekwa katika document ya mpango mkakati, ikiwa kutaonekana makosa katika utekelezaji; basi mashihisho yatapaswa kufanywa. Shughuli hii itapaswa kufanywa na mameneja wa ngazi zote za kampuni yako.
The Consult; +255 (0) 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania
Kwa huduma za
- Uandaaji wa michanganuo ya miradi (project proposals) na mipango mkakati (Strategic plans)
- Utoaji wa mafunzo (trainings) na ushauri (consultancy) katika maeneo ya usimamizi wa miradi (Project management) na mipango mkakati (Strategic Management)
Your Success is My Desire