TEMEKE- Hali ya barabara ni mbaya sana

TEMEKE- Hali ya barabara ni mbaya sana

ZINDAGI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
1,118
Reaction score
1,436
Najua wahusika wa barabara wanapita humu na viongozi tuliowachagua pia wanapita.
Hali ya barabara za Temeke ni mbaya sana kiasi kwamba kinasababisha foleni zisizokua za lazima.

1. Changombe Road, hii barabara ni moja ya barabara muhimu ya jiji, na inapitisha watu wengi wageni na wenyeji, cha kushangaza ni moja ya barabara mbovu inayofukiwa viraka kila mara na kuzidi kuharibika. Solution ni kuijenga upya tena kwa zege, eneo korofi kuliko lote ni kile kipande cha keko, leo tumetumia zaidi ya saa moja kupita kipande kile tuu

2. Mbozi road kipande kibovu kinachukua wiki tatu kukijenga huku barabara imefungwa, kipande hakizidi mita kumi, jiulizeni wale watu wa viwandani watafika vipi katika sehemu zao za kazi.

3. Barabara za mitaani zimegeuka mahandaki na parking za malori

Wahusika wa TEMEKE tubadilike.
 
Braza unakaa temeke ipo?? Ktk wilaya ambayo imefaidika kwa miradi mipya ya barabara Basi temeke haiwez kulalamika awamu hii,kqribia barabara zake nyingi zimeguswa kwa kiwngo kikubwa, na Sasa wanaendelea na ujenzi wa mwendo Kasi kilwa road,
 
Wahusika watafanyia kazi neno lako.
 
Kipande cha Veta mpaka Tameco hakujawahi kuwa na nafuu, hapa mvua hazijaanza. Zikianza aibu yake sijui tu. Ni sawa na kipande cha Studio mpaka Magenge Mwananyamala
 
Braza unakaa temeke ipo?? Ktk wilaya ambayo imefaidika kwa miradi mipya ya barabara Basi temeke haiwez kulalamika awamu hii,kqribia barabara zake nyingi zimeguswa kwa kiwngo kikubwa, na Sasa wanaendelea na ujenzi wa mwendo Kasi kilwa road,
Kwani hizo ni pesa za serikali?hizo pesa ni mradi wa WB, ndio maana ukienda hadi buza ndani ndani huko utakutana na maeneo tena sio lami tu, bali ni zege kabisa!!zinazoshughulikiwa na TARURA ni kama hizo za keko, ,na kutoka buguruni chama hadi mchikichini!!!ni vulugu tupu!!huo ulikiwa mradi mahususi kwa sehemu zenye wakazi wa kipato cha chini, nenda huko, kjichi ukaone!!
 
Mkuu hiyo foleni ya keko ni ya muda tu ni kutokana na kuruhusiwa gari toka barabara ya kilwa kuingia kutumia barabara ya chang'ombe ambako huko kilwa kuna matengenezo ya barabara ya mwendo kasi.

Foleni kuu ya hiyo barabara ni kuanzia pale mataa ambako kwa sasa kunajengwa fly over.
 
Najua wahusika wa barabara wanapita humu na viongozi tuliowachagua pia wanapita.
Hali ya barabara za Temeke ni mbaya sana kiasi kwamba kinasababisha foleni zisizokua za lazima.

1. Changombe Road, hii barabara ni moja ya barabara muhimu ya jiji, na inapitisha watu wengi wageni na wenyeji, cha kushangaza ni moja ya barabara mbovu inayofukiwa viraka kila mara na kuzidi kuharibika. Solution ni kuijenga upya tena kwa zege, eneo korofi kuliko lote ni kile kipande cha keko, leo tumetumia zaidi ya saa moja kupita kipande kile tuu

2. Mbozi road kipande kibovu kinachukua wiki tatu kukijenga huku barabara imefungwa, kipande hakizidi mita kumi, jiulizeni wale watu wa viwandani watafika vipi katika sehemu zao za kazi.

3. Barabara za mitaani zimegeuka mahandaki na parking za malori

Wahusika wa TEMEKE tubadilike.
Picha huwa kielelezo kizuri na muhimu sana kwemye mambo ya hivi
 
Barabara chini ya TARURA nyingi mbovu sana maeneo yote Tanzania.
 
Hii barabara haifai kwa matumizi ya Binadamu...mashimo yanaongezeka siku hadi siku, gari ndogo ni tabu tupu kupita pale.
 
Hatimae huu uzi umesikika, mkuu wa wulaya atoa amri barabara ya changombe eneo la Keko itengenezwe haraka sana.

Tunashukuru kiongozi kwa kutusikiliza kilio chetu.
 
Jioni hii nimekuta mitalimbo imeweka kambi pale na tayari washaanza kutekeleza agizo la DC
 
Back
Top Bottom