Mkuu
Sina habari za undani kuliko za kwako ila......mimi pia nililisikia kwa marafiki zangu 2 wa karibu ambao wanafanya kazi wazoefu kwenye mabenki 2 tofauti hapo Dar. Sikuwa na muda wa kuifuatilia sana ila walikuwa na wasiwasi kuwa huenda ni DECI ...hitimisho lilikuwa watajiandikisha na kwamba iwapo itatokea wakaliwa hela hiyo laki 5 kwao sio kitu.
Mazoa yasipopatikana inakuwaje? Tuseme wadaudu wamevamia shamba na kuharibu mazao. Market ya mazao isipokuwepo mwaka huo inakuaje?
Kwa mahesabu yangu hiyo laki tano inatakiwa izalishe 1.5 x 4 = 6 mil - 800,000= 5.2 mil + magunia 20 ya mahindi.
Ukubwa wa faidia ukifananisha na mtaji unanitia wasiwasi, lakini ni bora uongee na mtu ambaye amewahi kulima akueleze kama hizo faida zinawezekana kweli.
Kwa maelezo ya yule jamaa make nasema ilibidi waingie darasani wafundishwe na kuelekezwa itakavo kuwa, anasema hayo mashamba yatakuwa yanakatiwa bima, ya majanga kama hayo hata ya mabadiliko ya bei kuhakikisha kwamba mkulima hakosi hiyo 1.5 kwa heka moja!
Ukisikiliza maelezo (story behind) yanashawishi ila kwa vile wajanja wengi siku hizi ndo maana ni vyema kama kuna mtu anadata za uhakika wa hii kitu akazimwaga, ili kama ni kweli watu wachangamkie hizi nafasi.
Alisema wana na tangazo lao redioni linasema ''kwanini unahangaika kulima kwa jembe la mkono, nenda TOPPETA? watakulimia kwa trekta'', binafsi sijawai lisikia kwani huwa sifungulii sana hiyo Redio TUMAINI alo sema lipo!
Shotikati jamani!!!!!!!!!Dk.Remmy alisema ukinywa bia usipite vichochoroni....utakabwa...........!!!!!!MKULO,Ndulu vibaka wengine hao,wafakamie kama mwewe au kama helkopta ya Mbowe.🙂
Mapato ya jumla ya 1.7 au Milioni 1.5 net kwa mteja/mkulima kwa hekari ni faida kubwa mno. Sababu; wakati wa msimu wa mavuno wa Mahindi (kama mfano, sijui wao wanapanga kulima nini) kwa Dar kila gunia huuzwa kati ya Shs 5000 - 8000 vijijini/mashambani ni chini zaidi. Sijui bei ya mpunga wakati wa msimu wa mavuno kwa Dar au Mashambani (mwenye info tafadhali) atusaidie.
Kwa hesabu ya gunia 1 shs 8000 ili upate Shs 1.7 Milioni unahitani maguni 212 kwa hekari..!!! Au kama ni kuvuna mara 2 kwa mwaka basi kila mavuno upate Magunia 106 kwa hekari..!!! Huo utakuwa muujiza.
Najilaumu kwa nini sikuwafuata ofisini kwao niwasikilize kwa makini.
Naona kila mmoja anaongea kwa hisia na labda nyingi sana. mimi pia ninazo habari za huu mradi na nilienda ofisini kwao kueleweshwa vizuri.
Kwa kuwa kuna maswali mengi na majibu yake mengine ni more technical kwetu sisi sote na kwa kuwa mtoa mada anatoa pia ushauri kwa wanajamii kuchangamkia hii oppotunity, nashauri yafuatayo\;
1. badala ya kuendelea na hisia, wenye nia njema waende ofisini kwao karibu na mnazi mmoja jengo ambalo kwa chini kuna duka la top shop nafikiri ni ghoropha ya tano au ya sita.
2. Kuna darasa la kuelimisha watu wote wanaotaka kujiunga, maelezo ni bure na yatahusisha juhudi ambazo zimefanyika ikiwa ni pamoja na kulipima eneo lenyewe na namna ya umwagiliaji pamoja na namna mradi utakavyendeshwa kwa muda wa miaka kumi. Kuna issue pia ya masoko yaliyopo ya ndani na nje ikiwemo serikali kununua kwa ajili ya akiba ya chakula nchini.
Mimi sijapata hiyo laki tano lakini ikitimia tu nawahi mapema kwa kuwa nilielimika na nikapewa pia makabrasha yanayousiana na huo mradi. Naamini mradi huu usipoingizwa siasa unaweza kabisha kuliondoa taifa hili kwenye njaa inayojirudia mara kwa mara.

Mkuu,
Heshima kwako. Kwa sababu ulihudhuria darasa...naomba utupatie yale yaliyojiri huko japo kwa juu.
1. Mradi umeshaanza au unatazamiwa kuanza lini?
2. Mpaka sasa wana wanachama wangapi?
3. Nikilipa laki 5 na kuwa mwanachama, namilikishwa hiyo hekari 5 au nakuwa nimeikodi kwa kipindi cha mradi tu?
4. Ni gharama gani nyingine nitalazimika kuingia zaidi ya hiyo laki 5?
5. Uongozi mzima wa mradi ni wakina nani?
Ni hayo tu kutoka kwangu, tafadhali tuelimishe kwa jinsi ulivyuelewa wewe.
Ahsante
Mimi mashaka yangu ni hilo jina la mwenyekiti Dr. MUGISHAGWE linatia shakaKuna jamaa yangu kaniambia kwamba kuna hiyo association inaitwa TEDET (Tanzania Eco-Development Trust), kwamba inakusanya hela za wanachama kiingilio sh. laki 5 (500.000) ambayo inajumuisha kiingilio ada ya uanachama na shamba la ukubwa wa hekari 5 huko bonde la mto RUFIJI. Kasema makubaliano ni kwamba mwanachama anapewa hilo shamba heka 5, ila anakuwa analimiwa hilo shamba heka 4 mazao ya biashara na heka moja mazao ya chakula.
Mazao ya chakula atakuwa akipewa magunia 20 ya mahindi /mpunga kwa msimu yaani misimu miwili kwa mwaka, wakati mazao ya biashara yatakuwa yakiuzwa kwa pamoja masoko ya nje na kila heka ikikadiliwa kutoa mazao ya wastani wa thamani ya milioni 1.5, lakini mkulima atakuwa akikatwa laki 2 kila heka kama garama ya uendeshaji.
Kasema hiyo Tedeti inashirikiana na KIMUDEA umoja wa wakulima wilaya ya Kinondoni, na wakazi wa Rufiji chini ya umoja wao wa RUDIDEA na kwamba wanachama wanapelekwa kuonyeshwa mashamba huko Rufiji.
Nilipo search goggle nikakuta kweli hiyo kitu ilikuwepo toka mwaka 2006, na mwenyekiti wake ni Dr. Mugishagwe. Na kuna pesa mamilioni mengi, toka kwa wafadhili zimekuwa zikiingia huko TEDET, taarifa zipo ukigoogle za upokeaji wa pesa hizo. Hakuna taarifa zaidi kuhusu huu umoja, kilimo hata hizo ada za uanachama.. Kasema ofisi zao zipo MASASI HOUSE KARIAKOO?
Kweli nikaona maelezo yake ni mazuri, lakini nikapata hofu kwamba je hii haiwezi kuwa DECI ama PUFDEA nyingine? Manake hii kusanya ya kiingilio cha laki 5 kila mwanachama, na kasema wanatakiwa wanachama elfu 10,000. Na kasema wengi sana wamejiunga. Na ahadi ni kwamba wanaanza kilimo mwaka huu.
Ndipo nikaona pengine niimwage hapa kwenye Jamvi nene labda kuna wenye datas za uhakika nisije ingia mkenge wa DECI no.2
Na kama kweli si DECI, basi wanajamvi tuchangamkie uanachama kwani maelezo yake ni mazuri.
Asante wakuu.
Mod. tafadhali iacheni kwa muda hapa tupate datas
Mimi mashaka yangu ni hilo jina la mwenyekiti Dr. MUGISHAGWE linatia shaka