US anatumia economic pressure kwenye nchi ambazo anaona ni hatari kwa maslahi yake. Amerika tatizo lake anajiona yeye ni baba lao wa Dunia, sasa zikitokea nchi kama Russia, China,Iran n.k anaona ni kikwazo kwake. Hiyo ndiyo sababu Amerika anatumia economic pressure nia ni Ku' completing American tasks.
Sasa maamuzi mengine anayoyachukua ni mabaya hususan kwa nyakati alizokuwa nazo hizi. Kwa sababu Russia yapo makampuni makubwa ya Amerika ambayo yamewekeza kule, kampuni kama Cisco system inc, Apple inc, Pepsi Co, McDonald n.k: Kuweka vikwazo Russia makampuni yake nayo yanaathirika. Kingine ni kwamba, Russia haitokaa kimya tu na kutizama kuhusu sanction anazofanyiwa, eti na asifanye chochote(?) Hicho kitu hakipo.
What sanctions? Mwenzake Russia anajiimarisha sasa hivi, vitu wanavyomuwekea vikwazo yeye anakomaa anazalisha mwenyewe nyumbani. Kingine anatafuta ushawishi kwenye mataifa mbalimbali. Putin anazunguka sana sasa hivi, moja ya mizunguko yake ni kutafuta ushawishi. Kwa hiyo, ni suala la mahesabu tu. Ngoja tuangalie nani ni mwenye akili kubwa.