TCU YAFUTA VYUO VIWILI

TCU YAFUTA VYUO VIWILI

Mungoni Mshamba

Senior Member
Joined
Jan 30, 2017
Posts
154
Reaction score
63
Mwananchi
Vyuo viwili vyafutwa, vitano vyasitishiwa udahili
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) leo Septemba 25, 2018 imetangaza kuvifuta vyuo vikuu viwili, kusitisha kutoa mafunzo vyuo vikuu vitano na vyuo vikuu saba vikiwa chini ya uangalizi na kuagiza vyuo hivyo vinavyotakiwa kuwahamisha wanafunzi kutekeleza agizo hilo kabla ya mwaka wa masomo 2018/19 kuanza

Katibu Mtendaji wa TCU-Profesa Charles Kihampa akizungumza na vyombo vya habari leo, kushoto ni mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, Deus Changala
BY Harrieth makwetta, Mwananchi

IN SUMMARY

Advertisement

Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesitisha utoaji wa mafunzo katika vyuo vitano na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo katika vyuo hivyo kuhamishiwa vyuo vingine.

Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 25,2018 jijini Dar es Salaam amevitaja vyuo hivyo kuwa nChuo Kikuu cha Mlima Meru, Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB) na Chuo Kikuu cha Eckernforde Tanga (ETU).

Vingine ni Chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta- Kituo cha Arusha (JKUAT- Arusha Center na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCo) cha Bukoba mkoani Kagera.

“Vyuo hivi viko chini ya uangalizi maalum na hivyo hawaruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo kuanzia astashahada, stashahada, shahada, shahada ya uzamili hadi shahada ya uzamivu kwenye programu za masomo,” amesema.

Profesa Kihampa amesema TCU imevifuta vyuo vikuu viwili vya Theophil Kisanji cha Tabora na Mtakatifu Yohana cha Msalato jijini Dodoma.

TCU imeviagiza vyuo hivyo kuwahamisha wanafunzi kabla ya kuanza kwa mwaka wa masomo 2018/19.

Katibu mtendaji huyo amesema TCU imezuia udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika programu zote kwenye vyuo saba.

Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KIUT), Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian (MARUCo) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kadinali Rugambwa (CARUMUCo).

Vingine ni Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastina Kolowa (SEKOMU), Chuo Kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania- Kituo cha Marko (SJUT- St. Mark’s Center) na Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT).

“Vyuo hivi pia viko chini ya uangalizi wa Tume, vitaendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo na hawaruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo,” amesema Profesa Kihampa

“Tume imevitaka vyuo vikuu vyote vilivyotajwa kuzingatia na kutekeleza maelekezo. Tume inawaarifu wanafunzi wote wanaotakiwa kuhama kuwasiliana na vyuo vyao kwa ajili ya maelekezo kuhusu taratibu za kuhama na vyuo wanavyotakiwa kuhama.”
 
Mku tarifa i umeipatia wap
nawapongeza tume. lakini haitoshi. viko vyuo havina miundo mbinu inayoendana na idadi ya wanachuo.
Ila ajabu hiyo habari haipo kwenye website yako...naungana na newbiee01 kuhoji source ya mleta uzi japokuwa ni kweli kwamba vyuo vingine ni magumashi yaani kinachofanyika ni kupaka rangi administration block na kuandika "UNIVERSITY" alafu ndani hao wahadhiri michosho
 
Mku tarifa i umeipatia wap
Source hii hapa Mkuu
Screenshot_20180925-131544.jpeg
 
Nami nmeskia kwa radio ya nikwel wamefunga ila walichelewa mpka mamb ya udahili ya kuanza n ucmbfu kwq wanafunzi yan
 
St.John cha msalato ndo kipi hicho wakuu
Ni tawi la st.john kipo Msalato...kiufupi serikali ufute matawi yote ya st.john University ikiwepo main campus Mazengo kwani wameshidwa kuboresha miundombinu kulingana na idadi ya wanafunzi na pia hakuna wataalamu wa kutosha!

Mfano st.john mazengo campus mwanafunzi anayesomea masters mfano ya Education anafanya lecturing kwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea Education undergraduate kinachotokea hapo ni ubabaishaji tu na rushwa za kila aina!!!
 
VYUO SABA (7) VYASITISHIWA UDAHILI, VIWILI (2) VYAFUNGWA KWA KUKOSA VIGEZO:

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), imesitisha masomo na udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo na katika programu zote kwenye baadhi ya vyuo vikuu kutokana na kukosa vigezo.

Pia imefuta vituo viwili vya vyuo vikuu na kuamuru wanafunzi wanaoendelea na masomo wahamishwe mara moja.

Agizo hilo limetolewa leo Jumanne Septemba 25, 2018 ambapo Katibu Mtendaji wa TCU Profesa Charles Kihampa amevitaja vyuo hivyo kuwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini (KIUT), Chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU)-Tabora, Chuo Kikuu kishiriki cha Marian (MARUco) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kardinali Rugambwa (CARUMUCo).

Vyuo vingine ni Chuo cha kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU) kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Chuo Kikuu cha St. John cha Tanzania (SJUT)- Msalato Center na Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT).

Aidha, amevitaja vyuo vilivyositishiwa utoaji mafunzo na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo wahamishwe mara moja kuwa ni Mount Meru (MMU), Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB), Chuo cha Eckernforde Tanga (ETU), Chuo cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta Kituo cha Arusha na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCo).

“Asitokee mwanafunzi yeyote akasajiliwa katika vyuo hivyo na wanaotakiwa kuhama wawasiliane na vyuo vyao haraka,” amesema Profesa Kihampa.
 
St.John cha msalato ndo kipi hicho wakuu
Ni tawi la st.john.... linahusika mno na diploma lipo Dodoma msalato kule ....wewe wa Kikuyu utaendelea kupigana na coursework za kibabe
 
Ukweli umeongea lakn ntakuwa
Ni tawi la st.john kipo Msalato...kiufupi serikali ufute matawi yote ya st.john University ikiwepo main campus Mazengo kwani wameshidwa kuboresha miundombinu kulingana na idadi ya wanafunzi na pia hakuna wataalamu wa kutosha!

Mfano st.john mazengo campus mwanafunzi anayesomea masters mfano ya Education anafanya lecturing kwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu anayesomea Education undergraduate kinachotokea hapo ni ubabaishaji tu na rushwa za kila aina!!!

muhanga main campus Mazengo ikifungwa
 
Mwananchi
Vyuo viwili vyafutwa, vitano vyasitishiwa udahili
Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) leo Septemba 25, 2018 imetangaza kuvifuta vyuo vikuu viwili, kusitisha kutoa mafunzo vyuo vikuu vitano na vyuo vikuu saba vikiwa chini ya uangalizi na kuagiza vyuo hivyo vinavyotakiwa kuwahamisha wanafunzi kutekeleza agizo hilo kabla ya mwaka wa masomo 2018/19 kuanza

Katibu Mtendaji wa TCU-Profesa Charles Kihampa akizungumza na vyombo vya habari leo, kushoto ni mwakilishi wa Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo, Deus Changala
BY Harrieth makwetta, Mwananchi

IN SUMMARY

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) leo Septemba 25, 2018 imetangaza kuvifuta vyuo vikuu viwili, kusitisha kutoa mafunzo vyuo vikuu vitano na vyuo vikuu saba vikiwa chini ya uangalizi na kuagiza vyuo hivyo vinavyotakiwa kuwahamisha wanafunzi kutekeleza agizo hilo kabla ya mwaka wa masomo 2018/19 kuanza

Advertisement

Dar es Salaam. Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesitisha utoaji wa mafunzo katika vyuo vitano na kuamuru wanafunzi wote wanaoendelea na masomo katika vyuo hivyo kuhamishiwa vyuo vingine.

Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 25,2018 jijini Dar es Salaam amevitaja vyuo hivyo kuwa nChuo Kikuu cha Mlima Meru, Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UoB) na Chuo Kikuu cha Eckernforde Tanga (ETU).

Vingine ni Chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta- Kituo cha Arusha (JKUAT- Arusha Center na Chuo Kikuu Kishiriki cha Josiah Kibira (JOKUCo) cha Bukoba mkoani Kagera.

“Vyuo hivi viko chini ya uangalizi maalum na hivyo hawaruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo kuanzia astashahada, stashahada, shahada, shahada ya uzamili hadi shahada ya uzamivu kwenye programu za masomo,” amesema.

Profesa Kihampa amesema TCU imevifuta vyuo vikuu viwili vya Theophil Kisanji cha Tabora na Mtakatifu Yohana cha Msalato jijini Dodoma.

TCU imeviagiza vyuo hivyo kuwahamisha wanafunzi kabla ya kuanza kwa mwaka wa masomo 2018/19.

Katibu mtendaji huyo amesema TCU imezuia udahili wa wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo katika programu zote kwenye vyuo saba.

Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala nchini Tanzania (KIUT), Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Chuo Kikuu Kishiriki cha Marian (MARUCo) na Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Kadinali Rugambwa (CARUMUCo).

Vingine ni Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastina Kolowa (SEKOMU), Chuo Kikuu cha Mt. Yohana cha Tanzania- Kituo cha Marko (SJUT- St. Mark’s Center) na Chuo Kikuu cha Umoja wa Afrika Tanzania (UAUT).

“Vyuo hivi pia viko chini ya uangalizi wa Tume, vitaendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaoendelea na masomo na hawaruhusiwi kudahili wanafunzi wapya kwa ngazi zote za masomo,” amesema Profesa Kihampa

“Tume imevitaka vyuo vikuu vyote vilivyotajwa kuzingatia na kutekeleza maelekezo. Tume inawaarifu wanafunzi wote wanaotakiwa kuhama kuwasiliana na vyuo vyao kwa ajili ya maelekezo kuhusu taratibu za kuhama na vyuo wanavyotakiwa kuhama.”
Hiki kampala kifungiwe maisha kwanini hiki chuo kila majanga kipo.....ndugu zangu ambao mna ndugu zenu wanaosoma pale waondoeni haraka hakuna shule pale zaidi ya majengo
 
Back
Top Bottom