Nimeona baadhi ya matangazo ya baadhi ya vyuo vikuu ya kukaribisha maombi ya kujiunga na vyuo vyao kawa mwaka 2017/18.
Kuna taarifa muhimu hawatoi zinazomwezesha mwombaji kufanya maamuzi.
Taarifa kama: 1. Tuition fees 2. Administrative fees 3. Capacity for each course nk.
Taarifa hizi humwezesha mwombaji kujipima na kufanya tathmini kabla hajaamua kuomba chuo kipi na kozi zipi!
Pia vyuo vingelazimishwa kutumia online application ili kuwezesha mwombaji kufanya mabadiliko ya machaguo yake kabla ya tarehe ya mwisho na kuwa na uwezo wa kufuatilia wingi au uchache wa waombaji wengine kwa kozi mbali mbali.