TCRA yakana kurekodi mazungumzo kwenye simu

McCain

JF-Expert Member
Dec 2, 2016
1,169
517
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaonya watumiaji wa huduma za mawasiliano kuacha kutoa taarifa zinazowapa taharuki wananchi kuwa mamlaka hiyo imeanza kurekodi mazungumzo ya kwenye simu.

Akizungumzia ujumbe ambao unasambazwa kwenye mitandao ya kijamii, Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa TCRA, Semu Mwakyanjala alisema ni kosa la jinai kwa mtu kueneza taarifa za uzushi zenye lengo la kuibua taharuki miongoni mwa jamii.

Mwakyanjala alisema si kweli kuwa mazungumzo ya simu yanarekodiwa na TCRA, kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na haki ya mtumiaji wa huduma za mawasiliano.

“Mawasiliano ya simu ni masuala ya siri kati ya wahusika, sheria hairuhusu kusikiliza wala kurekodi mazungumzo, hata kama kampuni za simu zitatoa taarifa za wateja wao kwa mtu mwingine tunazichukulia hatua.

“Kama kuna suala la uvunjifu wa amani ambalo linatakiwa kufuatiliwa, basi kuna vyombo vya usalama ambavyo ndio pekee vinaruhusiwa kupewa taarifa hizo na si vinginevyo,” alieleza ofisa huyo wa TCRA.

Mwakyanjala alisisitiza kuwa maofisa wa TCRA wanafanya kazi kwenye ofisi za mamlaka hayo na si kwenye maduka au minada, na kuwa kama kuna mabadiliko au taarifa zozote, basi zitatolewa na ofisi husika itatoa taarifa.

Tangu juzi kumekuwa na ujumbe ambao umekuwa ukitumwa kwenye mtandao wa WhatsApp ikimnukuu mtu anayedai kukutana na ofisa wa TCRA wakiwa dukani na alimwambia kuanzia sasa simu zote zitarekodiwa hivyo wajihadhari na kuzungumza mambo ya uzushi ya watu wa serikalini au mambo yanayohusu siasa.

Ujumbe huo pia umezidi kueleza kuwa ili kujua simu inarekodiwa basi utasikia milio tofautitofauti kabla ya simu kuanza kuita.

Chanzo: Habari Leo
 
Afadhali bwana tulianza kuziona simu zetu kama mguu wa kuku,sasa full kujiachia.
2917848-1632275038-images.jpg
 
Vipi kuhusu tone inayosikika mara tu unapopokea au kupiga simu?
 
Kwani yule bwana wa Arusha mbona walisema wamepata ushahidi toka voda

Umeniwahi ndugu

ukienda polisi kuna kitengo cha tehama mfano hapa ngudu ukiingia kituoni mkono wa kushoto kuna TEHAMA je kazi yao ni nini?

angalizo: TEHAMA kirefu chake ni TEKINOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO sasa MAWASILIANO ni yapi?
 
Mnawekwa mtegoni kirahic ! Ss hivi nchi imegeuka,hakuna lakuamini wala wakumuamini.km ndivyo,mawacliano ya Ben Saa 8 na kupotea kwake mbona bado ni kizungumkuti? Ikiwa kuna wahucka maalum wakupewa taarifa?hili Lina walakini.wataingia waliomo na wacokuwemo.mf.kwann Maxmelo,alisumbuliwa km mitandao haifuatiliwi ? Au cm co mitandao ? Mtego wa panya huo !
 
“Kama kuna suala la uvunjifu wa amani ambalo linatakiwa kufuatiliwa, basi kuna vyombo vya usalama ambavyo ndio pekee vinaruhusiwa kupewa taarifa hizo na si vinginevyo,” alieleza ofisa huyo wa TCRA.

Taarifa hizo ni za aina gani? Na kumbukumbu ya taarifa hizo uchukuliwa wakati gani na nani?
 
Afadhali bwana tulianza kuziona simu zetu kama mguu wa kuku,sasa full kujiachia.View attachment 471222
Kama hawarekodi je, taarifa za uchochezi na yale majina feki ya wabugia unga walipataje na yule kijana walimpaje alipo jificha? Kumbe siku hizi ukitaka kujificha chomoa laini kwenye simu kabisa ndio ujifiche vinginevyohujajificha
 
sms ndio wanazionea sana mimi.nimeacha utuma sms natumia program za kuchat ambazo zina end to end encycription na natumia simu ambayo ina anti taping
 
Kama hawarekodi je, taarifa za uchochezi na yale majina feki ya wabugia unga walipataje na yule kijana walimpaje alipo jificha? Kumbe siku hizi ukitaka kujificha chomoa laini kwenye simu kabisa ndio ujifiche vinginevyohujajificha
Unajua kunajua kwa wale tulioishi kwenye mazingira finyu ukiwa na mkeo kwenye "shughuli" halafu,asubuhi mtoto wako anakuuliza, baba mbona mama alikuwa analia jana usiku?..si utamjibuje?
 
Back
Top Bottom