Aisee hawa jamaa kuna siku nimejiunga 1gb ndani ya sekunde zisizozidi 40 wameimaliza yote, nilipowapigia huduma kwa wateja wakanambia eti "tayari umeshatumia", nikawauliza nimefanyia nini maana nyie mnaona huko wapi nilitembelea na kupakua chochote!? Na nikawauliza, ina maana nyie siku hizi mna kasi ya 10G+ mpaka iwe chini ya dakika tayari imeshashusha/kupakua file lenye ukubwa wa 1gb!? Nikakosa majibu nikaambiwa tu tatizo lako limewasilishwa kwa wahusika watalifanyia kazi lakini kimya.
Mpaka leo sinunui vifurushi vya zaidi ya buku ili hata wakinifanyia uhuni isiniume sana.
Sent using
Jamii Forums mobile app