TCRA Simu yangu imeibwa nifanye nini?

fundi msati

JF-Expert Member
Aug 22, 2013
216
90
Habari wakuu wa jamvi,

Jana nilikuwa kwenye msiba wa nduguyangu huko Kongoe ya Dar, wakati tumemaliza majukumu muhimu tukawa tunajadili hili na lile na wengine wakiwa wanaendelea na mambo mengine ghafla akapita tukamuuona kijana tusiemfahamu ana anua nguo zilizo anikwa tukaanza kumfuata ili tumjue ninani, akakimbia na baadhi ya nguo chache akatokomea zake, sasa tuliporudi tukagundua kuwa ni mwizi na aliingia kinyemela mifuko ya wamama ilipekuliwa na kubeba vilivyomo na simu iliwekwa chaji nayo aliibeba, sasa nikakumbuka kuwa mamlaka ya mawasiliano ilituhimiza tuachane na visimu bandia nasi tukaitikia, leo hii simu ukweli imeibwa na nimewapigia watoa huduma wa mtandao wameniambia kuwa wao wanaweza kurudisha line tu.

Je nifanye nini TCRA na wenzangu mnaojua cha kufanya?
 
Kama unazo namba zake za utambulisho yaani IMEI ( International Mobile Equipment Identification) ukienda TCRA wataifungia, Kama huna hizo namba, basi samehe. Police lost report ni muhimu uwe nayo.
 
Asante kwa ushaur ninazo bhana nitafanya hivyo
 
Habari wakuu wa jamvi,

Jana nilikuwa kwenye msiba wa nduguyangu huko Kongoe ya Dar, wakati tumemaliza majukumu muhimu tukawa tunajadili hili na lile na wengine wakiwa wanaendelea na mambo mengine ghafla akapita tukamuuona kijana tusiemfahamu ana anua nguo zilizo anikwa tukaanza kumfuata ili tumjue ninani, akakimbia na baadhi ya nguo chache akatokomea zake, sasa tuliporudi tukagundua kuwa ni mwizi na aliingia kinyemela mifuko ya wamama ilipekuliwa na kubeba vilivyomo na simu iliwekwa chaji nayo aliibeba, sasa nikakumbuka kuwa mamlaka ya mawasiliano ilituhimiza tuachane na visimu bandia nasi tukaitikia, leo hii simu ukweli imeibwa na nimewapigia watoa huduma wa mtandao wameniambia kuwa wao wanaweza kurudisha line tu.

Je nifanye nini TCRA na wenzangu mnaojua cha kufanya?
Hii siyo 'platform' ya TCRA Tafadhali nenda ofisini kwao
 
Back
Top Bottom