TCRA na uzimaji wa simu: Ni sanaa, propaganda, utani au ufinyu wa teknolojia?

Nesto E Monduli

JF-Expert Member
Jun 6, 2016
247
155
Kwa Karibu mwezi mzima kumekuwa na Habari ya Kitaifa kuhusu Kuzimwa kwa simu feki.

Tukapewa na namna ya kuzitambua hizo simu feki kupitia mfumo wa namba za IMEI (International Mobile Station Equipment Identity).

Huu utaratibu ulikuwa unatambua IMEI ambazo ni "null" yaani hazipo kabisa na nyingine ambazo ni "duplicates" yaani zinashabihiana na simu nyingine ambayo ni halali. Tukaambiwa kutakuwa na uzimaji wa hizo kupitia mtambo au mfumo maalum na wa kisasa kuzinyima fursa ya kupata mtandao (Network Access).

Lakini kinachotokea baada ya muda huo kufika ni simu nyingi kuendelea kuwa hewani mojawapo nimeshuhudia mimi ambayo ina IMEI ya "duplicate" na jina la Darago lakini simu inaonekana ni "Nokia" zikiwa na model tofauti ,na kadhalika kutoka kwa watu wengine ambao walithibitisha kuwa simu zao zitazimwa.

Maswali yangu kadhaa ili kujua hili zoezi ni Sanaa,Propaganda, utani au Ufinyu wa Teknolojia mahususi ni kama ifuatavyo:-

1.Je Elimu haikutolewa vyema kiasi ambacho simu tulizojua zinazimwa hazikuzimwa?

2.Je Teknolojia ya mfumo wa kuzimia ina mapungufu ambayo yameufanya kushindwa kuzizima hizo simu?

3.Zoezi la uzimaji simu:TCRA hawakujiandaa au kufanya majaribio kabla ya kuchukua hatua?

4.Je hakuna siasa katika suala zima linaloendelea kuhusu uzimaji wa simu "Standardization" ?

5.Nini hatima ya wale ambao hawajazimiwa,Je simu zao ni halali kisheria au waendelee kukaa na wasiwasi? (Hapa naweka angalizo Isije kukawa na kesi nyingi za kuflash simu)

6.Maswali mengine Ongeza wewe!!!!!

---------------------------
Nesto E Monduli
Chanika,Dsm
 
Hahahhahha well said, hakuna simu iliyozimwa hata moja ya sample haipo ndio maana Innocent Mungy alikua hana poiny ya kusimamia, nilimsikiliza juzi Radio One Jioni anahojiwa yaani point alizokua anajadili ni hovyo sana na muda mwingi alikua anasubiri wasikilizaji wakioiga simu wakimsapoti ndio na yeye anapigilia humo humo
 
.. Lakini kinachotokea baada ya muda huo kufika ni simu nyingi kuendelea kuwa hewani mojawapo nimeshuhudia mimi ambayo ina IMEI ya "duplicate" na jina la Darago lakini simu inaonekana ni "Nokia" zikiwa na model tofauti ,na kadhalika kutoka kwa watu wengine ambao walithibitisha kuwa simu zao zitazimwa.
Weka IMEI hapa
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Wabongo maneno mengi hakuna kitu!, ujinga tu!. Kila kutupigisha umbea kila mahali eti simu zinafungwa simu zinafungwa, yaani mibaba na mimama inakaa kwenye viti inazungumza mambo yasiyowezekana. Zoezi lisifanikiwe kamwe nalaani zoezi kuanzia leo!!!!. Wapo kimya km sio wao walikuwa wanaimba kwa midomo hadharani tena kila siku
 
Mimi sina hamu kwa kweli.............!!
 
Kwa Karibu mwezi mzima kumekuwa na Habari ya Kitaifa kuhusu Kuzimwa kwa simu feki.

Tukapewa na namna ya kuzitambua hizo simu feki kupitia mfumo wa namba za IMEI (International Mobile Station Equipment Identity).

Huu utaratibu ulikuwa unatambua IMEI ambazo ni "null" yaani hazipo kabisa na nyingine ambazo ni "duplicates" yaani zinashabihiana na simu nyingine ambayo ni halali. Tukaambiwa kutakuwa na uzimaji wa hizo kupitia mtambo au mfumo maalum na wa kisasa kuzinyima fursa ya kupata mtandao (Network Access).

Lakini kinachotokea baada ya muda huo kufika ni simu nyingi kuendelea kuwa hewani mojawapo nimeshuhudia mimi ambayo ina IMEI ya "duplicate" na jina la Darago lakini simu inaonekana ni "Nokia" zikiwa na model tofauti ,na kadhalika kutoka kwa watu wengine ambao walithibitisha kuwa simu zao zitazimwa.

Maswali yangu kadhaa ili kujua hili zoezi ni Sanaa,Propaganda, utani au Ufinyu wa Teknolojia mahususi ni kama ifuatavyo:-

1.Je Elimu haikutolewa vyema kiasi ambacho simu tulizojua zinazimwa hazikuzimwa?

2.Je Teknolojia ya mfumo wa kuzimia ina mapungufu ambayo yameufanya kushindwa kuzizima hizo simu?

3.Zoezi la uzimaji simu:TCRA hawakujiandaa au kufanya majaribio kabla ya kuchukua hatua?

4.Je hakuna siasa katika suala zima linaloendelea kuhusu uzimaji wa simu "Standardization" ?

5.Nini hatima ya wale ambao hawajazimiwa,Je simu zao ni halali kisheria au waendelee kukaa na wasiwasi? (Hapa naweka angalizo Isije kukawa na kesi nyingi za kuflash simu)

6.Maswali mengine Ongeza wewe!!!!!

---------------------------
Nesto E Monduli
Chanika,Dsm
Si ufurahi kama hawajakuzimia?
 
Hakuna iliyozimwa hadi sasa!! Acheni urongo , propaganda za kisanii
Tangazo lao lilikuwa ni 16.06.2016 , Therefore kuna swali la tano pale kuwa Siasa zimeingilia hili zoezi?..
Kama Mpaka TCRA wanadanganya kwanye mitandao..Tuwashitaki kwa kutukanganya ?
 
Nilijua kuwa hii ni sanaa baadaya ya kusoma tahrifa ya TCRA jana wakidai kuwa ni 3% tu ndyo simu fake Tz wakan kila kona zimejaa. Tz inamaduka meng ya simu za kichina kuliko original. Na hya maduka ya simu za kichina ndyo yanaongeza ka mauzo.
 
labda walikuwa wanapromote simu za makampuni ya simu yauze,na kweli wa-make
 
Back
Top Bottom