TCRA msaada, nimechoshwa na SMS za moja spesho


anayeweza kukomesha hili tatizo ni TCRA peke yake (a.k.a baba mwenye nyumba)
 
Mimi najiandaa kuwashitaki nakamilisha jalada la vielelezo tu hapa wanakera kama nzi kwenye chakula
 
Waapuzi hawa asubuhi unaona meseji imeingia unastuka kwa mbwembwe ukidhani baby amekupa "gud morning my love" cha ajabu unakutana na Tatu mzuka...tena kila asubuhi
 
Mheshiwa Rais sio kak..nda peke yake muangalie na huyu waziri anayehusika na mawasiliano tumechoka na hii kero
 
Hivi hatuwezi kujiorganize tukawa fungulia jalada hawa watu
 
Hivi hatuwezi kujiorganize tukawa fungulia jalada hawa watu
Tufuatilie kwa wanasheria tuone uwezekano wa kufanya hivyo,na ninachojiuliza mimi hivi kwanini mamlaka husika hazishughuliki na malalamiko haya mpaka Mh.Rais aingilie kati,sijui nani aliyeturoga kutekeleza wajibu wetu mpaka tusukumwe.
 
Tigopesa yako ina jero. Leo ni siku yako ya ushindi. Instamoja hao na Mojaspesho
 
Kuna sms za nida,marufuku,muhimu,bet,mpesa ,bado za vifurushi yaan ni kero jamani kero kubwaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…