Tatizo ofisi nyingi za serikali siku hizi mpaka Mh. Rais aingilie kati,mwisho wa siku anaonekana kama anaingilia majukumu ya wizara au taasisi zake kumbe mabosi wangi wenye dhamana hawajitambui ukipishana nao koridoni wanatafuna tu hawajui hata nini wanapaswa kufanya.Mkuu TCRA wanatuangusha sana wananchi kwa hili la hizi sms za wachezesha kamari,yaani imekua kero kupita kiasi wapo tatu mzuka,mojaspesho,biko,instamoja, na wengine kibao.TCRA tusaidieni
Na hata huyo waziri mwenye dhamana akiambiwa ajitathimini kuhusu hili bado atajiona anatosha kabisa.Mkuu hii ni zaidi ya kero,binafsi per day napokea 10+ sms,mbaya zaidi nyingi zinaingia asubuhi,around saa 2-3,unaamka unaona simu inamwekua unajua una jumbe ya maana kumbe ni hawa wa bahati nasibu...pumb****v
Viongozi wetu wabinafsi sana,wanajali matumbo yao,familia zao,na watu wao wa karibu tu na sio kero za wananchi ambao kura na ufuasi kwao ndio umewaweka kwenye nafasi walizopo....hizi ndio siasa za AfrikaNa hata huyo waziri mwenye dhamana akiambiwa ajitathimini kuhusu hili bado atajiona anatosha kabisa.
Nunua Samsung Note(x) au Samsung S(x) au Iphone. Haipiti namba uki block.Kama kichwa cha habari kinavyojieleza nimechoka na sms zao nitumiwazo kila siku bila ridhaa yangu utadhani simu wameninulia wao ,Nimejaribu kununua simu janja nyingine jamii ya tecno yenye kaprograme ka kublock, nimejaribu kublock namba yao sms isifike lkn wapiiiii nimechocha sasa na hawa supa5 nao kero inaendelea,kuna kipindi mliwaambia walikaa kimya sasa hizi bahati nasibu za kulazimishana zimerudi kwa kasi,Kama itakuwa wameshindikana hawa watu wa michezo ya kubahatisha yenye kero ya sms basi tubadili mfumo turudi kwenye simu za upepo tuone sms watamtumia nani.
Kabisahata hawa Pesani mpesa wanaboa