TCRA hampaswi kuwepo duniani

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
24,638
Reaction score
30,262
TCRA ni msimamizi wa matangazo ya redio na runinga Tanzania, msimamizi anatakiwa kuhakikisha pande mbili anazosimamia zinapata haki sawa. TCRA imetoka kwenye usimamizi na kujikita kwenye mahakama zaidi kwa kukamata raia kwa makosa ya kipuuzi, kutoza faini vituo vya redio na runinga kwa mambo madogo.
Watumiajii wa redio na runinga tunapata matatizo mengi yahusuyo urushaji wa matangazo ambavyo TCRA wameyatelekeza, mfano kituo kama Startimes mitambo yake ilichoka huko uchina ikalrtwa hapa kama mitumba! Mvua ikinyesha inabidi tuhangaike na antenna ili tuone picha, pia uonekano wa picha kwenye TV haueleweki ni wa mfumo upi bahasha au sanduku (ratio) kinachosababisha picha isijae kwenye sikirini, ikitumia nusu au robo tu.
Katika awamu hii kukamata na kusweka ndani kunanoga zaidi lakini jaribuni kutukumbuka na sisi ingawa hakuna atakayeuona utendaji wenu.
Mwisho tumechoka kulipia picha zilezile miaka nenda rudi! Kila siku zinarudiwa rudiwa mwaka hadi mwaka, huu ni utoto.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…